Monday, January 5, 2009

HAPPY BIRTHDAY DAD

Tangu nabebeka kwa mkono mmoja
Mpaka sasa tusipobebeka. Baba bado ni Baba
Jonas Salk aliwahi kusema "Good parents give their children Roots and Wings. Roots to know where home is, wings to fly away and exercise what's been taught them."
Sijui ni mangapi unaweza kufanya ukahisi wamwakilisha mzazi wako na sijui ni mangapi yanakuendea vema ukaona na kutambua kisha ukathamini juhudi za wazazi wako. Kwangu ni mengi na ni kwa kuwa walisimama katika kile walichoamini ambacho japo enzi za utoto sikuona kama ni cha manufaa, lakini nilibahatika kutambua ni kiasi gani walikuwa, wamekuwa na wataendelea kuwa wa muhimu maishani mwangu na ndugu zangu kwa ujumla.
Nawazungumzia wote kwa kuwa uchaguzi wao wa kuwa pamoja, kuishi waishivyo, kuonesha msimamo wao katika maisha, kujihusisha na watu wa aina njema walioshirikiana nao, kuwa mfano katika matendo kwa namna waaminivyo na kuendesha maisha na namna walivyotuongoza mpaka kila mmoja kuwa alipo, ni kati ya "maisha" ambayo licha ya kuyatamani naanza kuyaishi japo katika tofauti za kimazingira na wanadamu wanizungukao.
Baba, umekuwa zaidi ya kioo cha maisha yangu na ndugu zangu kwa ujumla. Kunaweza kuwa na mengi ya kusema, lakini hakuna litakalozidi ASANTE kwa maisha uliyoanzisha, uliyowekeza na kuyadumisha kwetu. Tunatambua kuwa tuko tulivyo kwa kuwa kwa kiasi kikubwa mliwekeza mbegu bora utotoni mwetu na sasa twajivunia maisha tuwezayo kuishi kutokana na malezi yenu.
MAISHA BORA WAOMBEWA KILA SIKU, na usherehekeapo siku yako hii ya kuzaliwa, twataka mjue kuwa twajivunia kuwa nanyi kama wazazi na viongozi wa maisha yetu, na TWAWASHUKURU kwa kila jema mtendalo kwetu na jamii kwa ujumla

HAPPY BITRHDAY DAD

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ninakutakia heri, ya siku ya kuzaliwa,
Wewe u zawadi nzuri, duniani nimepewa,
Najisikia fahari, 'menilea nimekuwa,
Heri yako baba.

Mzee wa Changamoto said...

Dah! Asante sana Mtanzaga. Naamini kwa shairi hili ataweza kuona msisitizo wa umuhimu wa kile atendacho kwa wanawe.
Nami naamini nitakuwa hivyo kwa wana wangu.
Blessings

Simon Kitururu said...

Kushukuru ni bomba la kitu!Wengine hujisahau kwa kuwa tushaota mbawa na kuruka:-(

Heri ya siku ya kuzaliwa Baba ya Mzee wa CHANGAMOTO!

Christian Bwaya said...

Nimeipenda hii.

Wazazi ni sehemu yetu. Wana nafasi kubwa ya kutufanya tuwe kitu chochote. Inapotokea kuwa mwanao kawa kitu chema, bila shaka kuna kazi kubwa waliifanya.

Heri ya kuzaliwa baba! Alituletea 'kiumbe' wa muhimu sana.