Sunday, February 15, 2009

Filamu ya maisha, upendo na uathirika wa UKIMWI


Love in the Time of Aids from Lars Johansson on Vimeo.

Jana niliandika kuhusu hatua ambayo wanasayansi wamepiga katika kupambana na maradhi haya ya UKIMWI. Lakini pia kuna mambo yanayoendelea katika jamii nyingi na wengine wamepambana na kuzielimisha jamii mpaka wakaeleweka na kisha kupata ushirikiano mkubwa toka kwa jamii hiyohiyo.
Si wote waliopata ugonjwa huu kwa namna wanavyohisiwa na si wote wenye nia mbaya ya kueneza ugonjwa huu. Kuna weengi saana ambao wana moyo na wameamua kuelimisha jamii na kisha wanaishi MAISHA MAPYA, YENYE UPENDO, MATUMAINI NA IMANI kwa kuamua kujitangaza.
Tazama FILAMU hii niliyoipata kwa hisani / kutoka kwa Da Subi aliyoiweka katika toleo lake la Ijumaa tarehe 13 mwezi huu. Ni zawadi ya mafundisho ambayo kama una muda, TAFADHALI ITAZAME
ASANTE SAANA DA SUBI

3 comments:

Subi Nukta said...

Shukrani Mube kwa kuweka filamu hii kwenye blogu yako ili kuongeza uchaguzi kwa watu wenye nia ya kujifunza kutokana na video hizi. Kwa kweli ninatamani ingewezekana kushawishi vyombo vya habari kama vile Televisheni na Redio wakaweka filamu kama hizi ili kufikisha elimu hii kwa watazamaji wengi.
Shukrani za pekee zifikie Maweni Farm kwa kutengeneza filamu hizi na kwa wahusika wote waliodiriki kuwa vielelezo kwa simulizi za maisha yao.
Ninafurahia mawazo chanya ya namna hii.
Mube, kazi njema jirani!

Mzee wa Changamoto said...

Pengine nikushukuru wewe Da Subi kwa kuzisaka na kutuonesha. Nashukuru pia kuwa kuna wanaonieleza kuwa wameweza kuiangalia na HAPANA SHAKA kuwa wanajifunza kitu maana kama mtu ataiangalia hii na asiguswe basi atakuwa na mapungufu makubwa. Na uzuri ni kwamba haina taswira za kutisha lakini inafikisha ujumbe husika.
Shukrani kwako kwa mara ya tena Dada

Anonymous said...

Nime tazama na kufikiri mengi sn lkn mungu ni mkubwa wayote na nina himani kunasiku dawa zita patikana na walio kuwepo kwenye mateso wata ponyeka. mungu mkubwa