Sunday, February 22, 2009

MARAFIKI

Nakumbuka Kaka Bwaya aliwahi kuandika kuhusu urafiki, uhusiano na mpaka ndoa. Na nakumbuka tumeshaandika mengi kuhusu urafiki katika blog zetu za fikra. Lakini changamoto yetu iliyopo ni kutambua rafiki ni nani na suala hili laenda mbaali zaidi kwa kutambua UMUHIMU wa RAFIKI kwa rafiki.
Yapata wiki mbili zilizopita, rafiki yangu aishie mji jirani nami alinipigia simu na katika mazungumzo yetu alinieleza namna alivyougua ghafla na baadae akazidiwa akiwa nyumbani na kama ambavyo mimi nawe tungefanya, akawaita walio karibu ambao alidhani ni marafiki kuomba msaada wa kupelekwa hospitali, lakini kwa mshangao wake wengi walikuwa na "sababu" ya kutomfanyia hivyo. Aliniambia kuwa hilo "lilimfundisha na kumuonesha" nani ni rafiki.
Hivi punde RAFIKI ambaye pia ni DADA yangu alinieleza mawili matatu yanayomkabili na nikaamini kuwa nina wajibu mkubwa wa kujiweka katika nafasi yake na kuwa kwake kwa wakati huu na kujumuika naye katika magumu yake baada ya kutambua kile anachokabiliana nacho.
Na ndipo nilipotambua na kujiuliza kama kila mmoja anatambua umuhimu wa URAFIKI.
Beres Hammond ameuliza kuwa "Friends, what are you supposed to do? Should you build me up or break me down? Friends what are you there for, if in my needs you're never around. Friends what are your duties? Doesn't mean loyalty? Tell the truth even if when hurts, no matter what it may be. Cause I got my problems and you know that I got them and still you say nothing though you know I'm hurting"........" friends don't mean a thing if when I'm down you keep me down. Friends don't mean a thing, if I can't cry on your shoulder".
Nia hapa ni kuuliza kama kuulizana wajibu wa rafiki kama ni kukuzana ama kuangushana. Kama tunakuwa kimbilio la wenzetu wawapo na shida na kama tuko huru kukimbiliwa nao na kama tunajiona sehemu ya wao na kuwafanya wao kutambua kuwa ni sehemu yetu. Je tuna bega la kulilia kwa kila mmoja wetu? Kukaa kimya wakati rafikiyo ana tatizo ni kujiaminisha kuwa hana wakati analo. Kwako wewe unafikiri watimiza wajibu wako kama rafiki? Kwako rafiki ni yupi na upi wajibuwa rafiki?
Pengine kwa kumsikiliza Beres katika wimbo wake wa FRIENDS tunaweza kujiangalia kujua ni nani rafiki na upi wajibu wa rafiki na kama unafikiri kuna umuhimu wowote wa kuwa na rafiki kama "hakuna bega la kulilia" ama kuwepo msaada wa huyo umdhaniaye kana rafiki pale umhitajipo. MSIKILIZE HAPA

Pole Rafiki.

6 comments:

Subi Nukta said...

Kweli rafiki wa kweli ni yule anayekufaa nyakati zote, hasa zile za uhitaji uwe wa furaha ama karaha.
Rafiki ni bora kuliko mwanasesere!

Anonymous said...

Kuna changamoto kumfahamu/kumpata rafiki wa kweli! rafiki ni zaidi ya ndugu yako! sasa utamjuaje? wakati unapitia wakati ngumu na unamuhitaji!

Anonymous said...

Rafiki wa kweli ni yule akufaaye wakati wa dhiki na siyo tu mwisho wa mwezi. Ukiugua, nyumba yako ikiteketea kwa moto (au kuchukuliwa na mdeni wako) na misukosuko mingine ya maisha ndiyo utajua yupi ni rafiki na yupi ni mtumiaji!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sio wakati mgumu ndo rafiki aje. mbona kuna marafiki kibao kabla ya wakati mgumu? rafiki anakufaa wakati mzuri endapo wewe ni rafiki yako.
ukiwa rafiki yako mzuri kwako wewe mwenyewe, basi utapata marafiki. kiutambuzi hakuna wakati wa shida wala wa raha kwani nyakati zote ni sawa. ni upi mzuri au mbaya ni tafsri yako mwenyewe.

hakuna kitu kibaya maishani na kama wewe unasubili rafiki akufae wakati wa shida, basi humpti ng'o kwa sababu nyakati zote zitakuwa ni za shida kwako kwa sababu unamsubili irafiki atokee.

ndio maana wengi mnajiita marafiki wa yesu msiyemouna na kujifanya maadui wa kamala mnayemuona. mshindwe

Anonymous said...

Kamala, hiyo taaluma yako ya utambuzi mhh... Kazi kweli kweli! Nawahurumia watoto wako (kama unao). Kama huna pengine ni bora usiwe nao...Nawahurumia pia hao wanaofika kwako kupatiwa huo utambuzi kwani kwa kweli itakuwa unawaTUMBUZISHA kisawasawa. Bakia ngangari baba!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony. kwa nini nisiwe na watoto? mke wangu ananipenda sana kwa sababu ya nilivyo yaani hatuwezi kugombana wala nini kwa sababu kila kitu kwangu ni simpo. watoto hata wa mitaani hunifagilia kinoma kwa sababu nawaheshimu na kuwapokea kama walivyo