Saturday, March 7, 2009

Tunazidi kujipoteza katika harakati za kujitafuta


Umeshawahi kutafuta usichojua ama kutafuta ujuacho usipopajua?
Je kujaribu kujitambua kwa kujipoteza mwenyewe?
Labda sieleweki!!!!
Umeshawahi kuwaona wale ambao mbele ya nyuso fulani wanaweza kufanya mambo ya ajabu ili tu waonekane wao ni bora mbele ya hao wajioneshao kwao?
Wanaoweza kuwatesa wenzao ili tu kujionesha kuwa wana ubavu? Wanaoweza kutenda ya kipuuzi ili tu waoneshe kuwa wanakwenda na wakati!!
Nakumbuka mwaka 2003 nikiwa Manzese na joto likiwa kali mchana kweupe nilishuhudia kijana mmoja ambaye alikuwa msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya (mwenyewe alikuwa akidhani anaimba rap) na ambaye alikuwa amevaa nguzo zinazofanana na za mwanamuziki mmoja wa Marekani aliyekuwa akivuma wakati huo. Hiyo haikuwa tatizo, ila zile zilikuwa ni nguo za majira ya baridi na ambazo mwanamuziki huyo wa Marekani alizitumia kwenye video yake ambayo yaonekana wazi kuwa aliirekodi wakati wa majira ya baridi. Lakini kwa kuwa msanii huyu chipukizi alikuwa kwenye harakati za kuutafuta umaarufu ama kujitafuta mwenyewe kwenye kundi la wana-hip hop, akajivalisha leather jacket mchana kweupe joto likiwa kali. Nilijiuliza mateso anayopitia ndani ya mwili wake ili tu kuvuta "attention" ya walio nje.
Ndivyo ilivyo kwa maisha ya sasa.
Watu kutenda yasiyotendeka ili mradi tu wanataka kujidhihirisha kuwa nao wana uwezo. Nchi zinavamia nchi nyingine ili "kutuma ujumbe" kwa wengine kuwa wasithubutu kuwa kama wenzao. Viongozi wanasitisha huduma kwa baadhi ya sehemu kwa kuwa tu hawakupigiwa kura sehemu hizo. Watu wanaotoa utu na kutenda mauaji kwa albino ili tu kutafuta nafasi ya maendeleo maishani mwao. Madereva ambao kwa kutaka kudhihirisha kuwa nao wamo kwenye kuendesha wanakwenda zaidi ya mwend kasi wa kawaida na kuishia kuua wasio na hatia.

Kuna haja gani ya kutokuwa sisi?
Kuna umuhimu gani wa kutenda yasiyotendeka ili mradi tu kutaka ku-send message kuwa nawe umo?
NI UPUNGUFU GANI UTUFANYAO SISI KUENDELEA KUTENDA TUTENDAYO NA AMBAYO TWAJUA KUWA HATUSTAHILI KUTENDA LAKINI TWATENDA KUWARIDHISHA WENGINE?
INASIKITISHA, MAANA
TUNAZIDI KUJIPOTEZA KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA NA KUDHIHIRISHA KUWA SISI NI NANI NA TWAWEZA KUFANYA NINI.
Naacha!!!!! Tukutane "Next Ijayo"
Msikilize Ziggy Marley ambaye naye katika sentensi yake ya kwanza anaukiza "why we lose ourselves just to find who we are"?

4 comments:

Anonymous said...

Ama kweli we mzee wa changamoto!

Yasinta Ngonyani said...

hapo kazi ipo kweli kweli. jmosi njema kakangu.

Simon Kitururu said...

Kazi kwelikweli!

Christian Bwaya said...

Kuna haja gani ya kutokuwa sisi?
Kuna umuhimu gani wa kutenda yasiyotendeka ili mradi tu kutaka ku-send message kuwa nawe umo?

Naam. Umenena.