Wednesday, April 29, 2009

Enziiii. Tunapoteza nini tunapoongeza nini?

Enzi zangu. Hii ilikuwa ni "one shot" baada ya maandalizi ya kutosha. Hahahahaaaaa. Back in time.
Kwa miongo miwili iliyopita kumekuwa na mabadiliko makubwa saana ya teknolojia. Nakumbuka "enzi" hizo mambo kama kupiga picha ilikuwa ni suala la miadi na mpigaji (kama hukuwa na kamera ndani na naamini wengi hawakuwa nazo), kisha unafanya "zoezi" la style halafu akija unapiga na kusubiri kwa muda (kulingana na ulipo) kabla hujapata picha yako. Nadhani hii ilitufanya tuwe makini saana maana hatukutaka kupoteza picha ama kupiga piucha ambayo tutalazimika kuilipia hata kama hatuitaki.
Lakini sasa kwa teknolojia iliyopo, unaweza kupiga picha 1000 kisha ukachagua moja ya kutumia.
Hivi hatujapoteza kitu kutokana na teknolojia hii? Pengine "za kale" zilitupa maandalizi mazuri katika kujiandaa kupiga picha na mengine mengi ambayo sasa tunayaweka pembeni kwa kuwa tu kuna "teknolojia". Hatutumii ramani tena, tunategemea GPS, hatupiki, ni fast food tuuu. Hatunywi maji yenye usafi wa asili, bali twataka kununua yaliyochujwa toka kwenye maji taka. Hatutembeleani, ni email na jumbe fupi na simu. Hatuaminiani, kila kitu ni kwa "wino wa mashahidi". Hatupendani kwa dhati, mwenye nacho ndiye apendwaye. Yaaani ni mabadiliko kwa kwenda mbele (japo yaturudisha nyuma)Mambo mengi tuyaonayo ya kizamani hunirejesha "back in time" MSIKILIZE INNOCENT GALINOMA HAPA KATIKA WIMBO WAKE ALIOUITA BACK IN TIME

13 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapo umesema Zamani kila kitu kilikuwa ni safi sana. Siku hizi kuna mambo mengi; ila maendeleo hayaonekana kabisa kwani sasa ni kweli watu tumeacha kutembeleana hapa na hapa tu unapiga simu badala ya kwenda. Nadhani hii pia inasababisha watu wengi kuingia katika lile kundi la kunenepa kupita kiasi. Picha za zamani ni nzuri sana nimekapenda kakijana haka. Kwani binafsi sina picha kama hiyo ya "Enziiii". Ahsante kwa mada hii

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

wanyujikya harai mara bingi. kwijakutelwa epicha lazima mwoge, majwalege mwesig'amajuta, mwagya ambala bala, mya, myai, mwagilinda eilimansi lyona
olundi mbabalazimisha kusheka!!!

tehe tehe

Mzee wa Changamoto said...

Ni kweli Yasinta.Kwanza haka ka-kijana ndiko kanakokujibu sasa hivi. Hizo ni enzi zake. Ilikuwa safi saana japo nilikuwa nikichukia maandalizi yake maana yalikuwa yakinikatisha michezo. Naamini ndio maana mara nyingi watu walikuwa wakipiga picha siku zao za ibada na wapiga picha walikuwa wakivizia watu wakitoka kwenye ibada kabla hawajachafuka wanapiga picha.
Ni kama asemavyo Kaka Kamala kuwa wakati mwingine (mara nyingi jumapili jioni) unaogeshwa na "kusilibwa" mafuta kisha mwaenda "center" ya kijiji kusubiri picha mlkiyokuwa mkiisubiria kwa juma zima.
Kuna mengi ya kukumbuka na kuenzi

Christian Bwaya said...

Kaka hii safi. Haha ha ahaaa!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Umenifanya niitafute albamu yangu ya kumbukumbu. Kuna picha ambazo mtu hata ulibidi upeleke suruali uliyoipenda kwa fundi cherehani ili airekebishe vizuri ili uje utoke pyua kwenye picha. Zipo zingine nilipiga katika ofisi ya mkuu wa shule kule Kahororo Sekondari. Maandalizi yako wazi. Ni kweli dunia imebadilika - maisha haya ya ipod, iphone, nintendo wii na Blackberry kweli ni hatari. Sijui tunaelekea wapi? Hapa naungana kabisa na Kamala kwamba pengine mtu yule aliyeko kijijini mgombani ana maisha yenye ridhiko kuliko sisi ambao kwa kutojua kwetu tunadhani kwamba tumeuchinja kumbe tumechinjwa/tunajichinja!!!

Halafu Kamala - hicho Kihaya kimenitoa knockout kabisa. Aisee hata Kihaya changu kumbe kimeshapotea tayari wakati kipindi fulani nilikuwa na uwezo hata wa kum-convince mwisiki mpaka akakubali kuwa mkazi wange kwa kutumia Kihaya tu. Nimesikitika!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo!!! duhuuuuuuuuuuuu

ninkushaba engozi kaisiki, kolayanga otwala kaisiki, abaisiki baijwile kaisiki.

hiyo ni sehemu ya mistari ya enzi hizo ya ku-convince kaisiki

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kamala, nimeshakwambia kwamba Kihaya changu kimeshakufa. Hebu tutafsirie huo ubeti/msemo ili tufaudu...

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaaaa. Duh!!! Hii kali. Kamala anamwaga "beti" za ki-poripori hapa. Raha saaana. Ila mnajua kuwa hata watumiaji halisi wa lugha za kiasili wanazidi kupungua? Yaani wengi ukiongea nao watasema kuwa wanaweza kuongea ama wanasikia lakini hawawezi kuandika. Tunapoteza kizazi

Yasinta Ngonyani said...

Mmh hapo kali ingawa sielewi kitu ila nafurahi sana kuona watu wanaopenda/ongea lugha zao za asili HONGERA Kamala. Lakini kweli tafsiri ili tufaizi wote

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kamala, jamaa mmoja Mkurya - wakati ndiyo tu tumekaramka tukiwa kidato cha pili alijaribu kum-convince mwisiki kwa maneno ya busara. Alianza kwa kumwambia kwamba yeye hana maneno mengi kwani "...ebigambo bingi bikatanga enkoko okwikukusa..." Basi mpaka leo bado naikumbuka hii methali. By the way, mwisiki alicheka tu na kwenda zake! Sijui alichemsha wapi! Tunasubiri tafsiri ya huo ubeti hapo juu.

Unknown said...

Unanikumbusha mbali sana enzi za primary sasa inapopigwa picha ya pamoja lazima mtu utoe alama kama kunyosha kidole maana unaweza usijijue picha ikitoka na zile uniform basi inakuwa kazi kwelikweli.

Ila tutoto twa siku hizi twenyewe ndo fundi kupiga picha.

Ila hapo mzee ulitulia si utani, Hongera sana

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

haya maatondo, natafsiri kwa sharti moja kwamba na wewe utwambie nini maana ya majina yako matatu.

'naukomba mapensi ki-sichana, ukataa potelea mbali kisichana kwani wasichana ni wengi na wamejaa tele'.

hiyo ya ebigambo bingi bikatanga enkoko okwikukusa... maana yake ni, 'maneno mengi yalimfanya kuku asahau kuchamba'

yaani inapendeza sana kukumbukia nyumbani ehe? nilikuwa kijijini na wazee, nilifurahi kurudi home na kukipiga kikwetu sana.

blog ya kikwetu ipo njiani kuanzishwa, matondo utakuwa mtazamaji au mchangiaji?

Koero Mkundi said...

haka ka mdahalo kalinipita.
Nilikuwa najiuguza malaria huko Arusha.....
Duh nimepitwa na mengi?
Nimekuona mzee kumbe ulikuwa handsome tangu utoto.....
ha ha haaaaaaaaaa.......