Friday, April 17, 2009

Them, I & Them.. PETER TOSH .......Equal Rights

Wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na wimbo la mauaji ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na tulishuhudia karibu viongozi wote wa serikali wakipiga vita UKATILI huo uliokuwa ukifanywa na WAHALIFU wasiojali uhai wa wenzetu. Ambacho sikusikia ni tafsiri yao ya Mhalifu. Tumewasikia wanasiasa mikutanoni wakizungumzia RUSHWA japo hawawezi kukupa tafsiri ya mla rushwa wala kukwambia mla rushwa ni nani. Tumewasikia wanasiasa wakituambia walivyo na nia ya kutuletea maendeleo japo hawaonekani kujua umbali tuliopo toka yalipo maendeleo hayo mpaka tulipo. Pia kuna "waamini" wanaoijua na kuipenda mbingu na ambao wanajua huifikii mpaka ufe, lakini licha ya kuwa wanataka kwenda Mbinguni, bado wanaogopa kifo. Na mbaya zaidi, tunawasikia na kuwaona wanasiasa hawa hawa wakijadili na kutaka AMANI wakati hawawapi wananchi HAKI NA USAWA.
Nakumbuka Dennis Brown aliwahi kuimba akisema "sitting and watching fools by themselves when they should always thinking of getting to know themselves."
Linalotakiwa ni KUJITAMBUA. Kutambua kuwa wanakimbia kivuli chao wenyewe na kusaka wanachokificha.
Naacha.
Na tuungane naye PETER TOSH akitufundisha, kutuelimisha na kutupa ukombozi wa kiakili katika wimbo huu mwanana uitwao EQUAL RIGHTS

Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)

(CHORUS)
I don't want no peace
I need equal rights and justice (3x)
Got to get it
Equal rights and justice

Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die

CHORUS
(Just give me my share)

What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I

CHORUS
(I'm fighting for it)

Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom

CHORUS

Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them

CHORUS

There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Jamaica


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment: