Tuesday, May 19, 2009

Hesabu za kisiasa

Mara zote ni kinyume; wengi ndio wachache na wachache ndio wengi

Hivi ulibahatika kusoma toleo la Kaka Kamala alilosema MOJA JUMLISHA MOJA SAWA NA MOJA? (BOFYA HAPA KAMA ILIKUPITA). Je maoni ya waliochangia akiwemo Ndugu Born Again Pagan?
Kuna ukweli wa hesabu za wenzetu hawa wanasiasa ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa kinyume na zile tulizozoea kwenye masomo na elimu yetu ya kawaida. Kwa ni kama wengi wanakuwa wachache na wachache wanakuwa wengi. Hakuna kujali kile wanachoimba na kuahidi kukitetea wakati wa kampeni zao. Hawawajali wananchi na kwao ubinafsi ni maana nyingine ya "manufaa kwa umma"
Labda tuangalie UMOJA WA MATAIFA ambao una wanachama lukuki na unaonekana "kutawala" dunia kimaamuzi lakini bado maamuzi ya mataifa matano yenye kura ya turufu ndiyo yanayoamua dunia iende wapi, iadibike na / kuadibishwa vipi, nani awe rafiki wa nani na nani awe adui wa nani hata kama hawana jibu la kwanini iwe hivyo. Na mataifa mengine yanatulia na kuendelea kutafsiri hiyo kama DEMOKRASIA.
Tukirejea kwenye ngazi ya nchi, tunaona kuwa maslahi ya wananchi pengine ndio kitu cha mwisho kufikiriwa akilini mwa "waheshimiwa" hawa. Wanatanguliza u-mimi na hata maamuzi yao hayaonekani kuwajali wengi ambao ndio waliowachagua. Hawawajibiki, hawaonekani kuwathamini na hawako katika nyadhifa zao kushughulikia lolote lihitajiwalo nao. Kwao, kulinda heshima yao ni jambo la muhimu kuliko kujali wananchi. Wanasikia matatizo, wanayaona na kisha WANAYAPUUZA
Nasema mahesabu yao yako kinyume maana kwao wananchi ndio "minority." Kwao wanaona kama wanahitajika kumaliza mahitaji yao kwanza ndio njia sahihi na ndio maana kwangu mimi ni WATAWALA kuliko viongozi.
Sasa kwanini tunawaamini? Kwanini tunawapigia kura wakati hatuna nafasi kwao kwani jamii nzima kwao ni "minority."
Wasikilize Morgan Heritage katika kibao chao hiki, POLITICIAN hasa wanaposema "why should we trust politicians, why should we vote every election? When there's no place for we, you and me, in the secret society they call us minority."

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio maana siku zoote sipendi siasa na nazichukia siasa na wanasiasa japo nalazimika kuishi kwenye jamii inayoongozwa na wanasiasa

ujinga wa namna hii ipo siku utakwisha tu labda ndio maana halisi ya democrasia.

asante kwa uthibitisho wa hesabu juu ya moja na moja ni moja

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli hata mimi sielewi kwa nini tunalazimika kuwapigia kura watu tusiowafamu kama wanaweza kazi hii. Naweza kusema mara nyingi tunapiga kura kwa sababu wanapita mitaani/vijijini na hizi kampeni zao wanatoa kanga, T.shirt na kama mwaka huu nilipokuwa nyumbani walikuwa wanatoa mbolea za kampeni. Hii yote ni ujinga tu kwani wao wanataka kuwavutia wananchi tu. Je? hii ni halali? kwani pale inakuwa wanalazimisha kupata kura. Nami natumaini siku moja kutakuwa hakuna mambo haya.

Mija Shija Sayi said...

Kamala naikataa kauli yako kwamba..'.."ipo siku ujinga huu utakwisha tu".., Mimi nasema sidhani kama siku hiyo ipo. Naomba utetee hoja yako, Kwa vipi unadhani ujinga huu utakwisha na mimi nitakwambia kwa vipi ujinga huu sidhani utakwisha. Nawasilisha hoja Mzee wa changamoto.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

elimu na umoja ni tiba mbadala wa kupambana na wachuuzi wa siasa.


elimu ninayoongelea hapa sio kupewa lekcha au kuandikiwa ubaoni na ticha.

ni elimu ya mtu kutambua kuwa 2 mammbo kamwe hayawezi kutoa maziwa nchi nzima"

tukingamua hilo naamini tutafika mbali.binafsi sina ubaya na 'politiki' ila nina tofauti kubwa na asilimia kubwa ya waliovamia siasa...

pumzikeni mlikotangulia wanaharakati wa kweli..wana wa afrika na wanasiasa wa kweli..

tutafika tu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ubinadamu, utu na umoja ukitawala, basi ujinga huu unaoongozwa na uroho utakuwa hauna nafasi tena

malkiory said...

Mzee wa Changamoto,

Hapa moja kwa moja umewalenga Wabunge wetu wa Tanzania pamoja na speaker wao ambao kwa pamoja walilaani vikali kitendo cha Slaa kuanika maslahi yao. Chakushangaza zaidi ni pale ambapo waziri mkuu alitamka hivi karibuni kuwa anatarajia kuboresha maslahi ya wabunge kwa madai kuwa wanataka kuongeza utendaji kazi wa bunge.

Inashangaza kuona hata wabunge wa upinzani walimgeuka Dr Slaa pale tu alipoanika maslahi yao hadharani. Je kama serikali inaelewa kuwa kuongezeka kwa maslahi unaenda sambamba na utoaji bora wa huduma kama alivyosema waziri mkuu, sasa kwanini huu uboreshaji wa maslahi uwe kwa wabunge tu? wakati wafanyikazi wengine wa serikali wanapata maslahi duni kupita kiasi!