Friday, June 26, 2009

Them, I & Them ...ECHOES OF MY MIND ......Luciano

Alipoamua kuingia katika katika NBA Draft, wapo waliosema mengi wakimtisha kuwa hakuwa tayari na pengine kulikuwa na uwezekano wa kutochaguliwa. Lakini hilo halikuwa mawazoni mwa Hasheem Thabeet ambaye aliendelea kuamini kile kilichokuwa akilini mwake na kuendelea kusikiliza MWANGWI WA MAWAZO YAKE. Napenda kumpongeza kwa kuamini katika alichoamini kwa kuwa kilikuwa sahihi na kilipaswa kuaminiwa na hakuna kitu kizuri kwa mtu kama kuwa vile anavyotaka kuwa. Na Hasheem amefanya hivyo kwa kusikiliza mwangwi wa mawazo yake na kufuata ndoto zake.
Kila la kheri Hasheem.
Msikie Luciano katika wimbo huu ECHOES OF MY MIND ambapo anasema si wakati wote unatakiwa kusikiliza kile ambacho wengine wanasema, bali sikiliza mwangwi wa mawazo yako.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

Subi Nukta said...

Nakubaliana na ulichosema Mubelwa.
Siku zote ni kupanga vyema na kufuata mipango hiyo kwa makini.
Ninamwombea mafanikio mema kwake na kwa wale wote watakaonufaika kwa mafanikio yake.
Hongera sana Hasheem!

Yasinta Ngonyani said...

Namtakia mafanikio mema pia na pia Hongera sana.

Anonymous said...

Mzee unajua kuhusisha matukio. bomba kweli yani