Sunday, August 30, 2009

Give Thanks and Praises....PROPHECY by Luciano

Maisha tuishiyo sasa huonekana kutawaliwa na wale watuzungukao ama pengine maisha yatuzungukayo na mwisho wake tunashindwa kuipata ile KWELI iliyo ndani mwetu na ambayo inastahili kuendesha maisha yetu. Ni sababu hiyo hiyo inayomfanya mtu kuogopa kutenda yale ambayo angeweza kutenda kama angekuwa na mtu mwingine. Hii inamaanisha kuwa tunatawaliwa na uoga kuhusu tutakavyomaliza maisha yetu kuliko uhalali na usahihi wa maisha tuishiyo.
Leo ninaye Luciano ambaye katika wimbo huu anaanza kwa kutufunza kuwa haijalishi tuko wangapi, kama ni wakati wa mmoja kuondoka basi ataondoka na pia kutuusia kuwa wenye busara "wanatazama na kuomba" katika nyakati hizi. Anasema "two shall be sleeping and one will be taken away. In this trouble times the wise MUST watch and pray. The light go shining yet still fools go astray. Guarantee not to them is another day"
Anaendelea kutuusia kuhusu HUKUMU za yale tuyatendayo na ambayo wakati mwingine twayatenda tukiwa na "support" ya wenzetu ambapo anasema wakati wa hukumu hao hawatakuwepo.
Maono haya aliyonayo Luciano na suluisho analotupa, ndivyo vitu vilivyopo duniani sasa. Kiitikio chake anasema "see there's death and destructions taking all over the land. And WARS and confusions taunting the HEART of men. But there will be PEACE AND SALVATION for the Righteous men. REJOICING AND REDEMPTION for the CLEAN HEARTED ONES."
Anatuasa mengi kuhusu HUKUMU ya mwisho kuwa wapo watakaokimbilia miamba nayo itawalilia kuwa hakuna pa kujificha, watakimbilia milimani nayo itaporomokea baharini na namnukuu akisema "some will run to the rocks, and the rocks will cry out THERE'S NO HIDING PLACE HERE. Some will run to the mountains and the mountains will crumble into a sea of dispear"
Msikilize wakati ukifikiria namna ya kubadili maisha yako

JUMAPILI NJEEEEEMA!!!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

jumapili njema kwako na familia yako.