Friday, October 2, 2009

Them, I & Them....BUJU BANTON ...Close One Yesterday

My DEDICATION to all who are in need, who are being Downpressed, Tortured, Poor .......
Maisha tuliyomo twayaona namna ambavyo YANAPOTEZA UHALISIA wa uhitaji na kuendeshwa na wenye sauti ambao ni wenye uwezo. Hali ya sasa katika nchi nyingi (ambazo zimeharibikiwa na mifumo yao ya siasa) tunaona namna ambavyo wachache wenye nacho walivyo na uweingi wa sauti na maamuzi.
Haya yapo duniani kote na haionekani kama kuna unafuu popote. Na Blog hii ambayo imekuwa sauti ama mwakilishi wa wenye changamoto, inaendelea kuwaeleza wale walio katika hali za kukandamizwa, wenye uhitaji na wanapuuzwa, wanaogumishiwa maisha yao na wenye uchu, wanaoibiwa haki zao, wanaolazimika kununua haki zao na wanaonyanyaswa kwa namna yoyote kuwa kuna asiyefanya maamuzi kama hawa wenye nacho ambao wanajitahidi kujisahaulisha kuwa maisha waliyonayo si ya kudumu. Kama Buju asemavyo kuwa "be not grieved riches are not forever, envy not the opressor choses none of his ways, be not wise in his own eyes only JAH you must praise"
Anawagusa na WATAWALA wetu ambao kwa namna moja ama nyingine wameamua KUHALALISHA UONGO kuhusu maisha yetu kama vile hawaoni tunavyotaabikwa kwa makosa yao anaposema "This nine to five is a joke Compare to the pressure, The minister say "The economy is getting better", Misleading the people the mass still suffer, Oh Jah Scarce benefits and spoils. Jah know that we feel it. Day and night we cry, cry, cry " na anasema japo yaonekana tunaporomoka na wao (matajiri) wanazidi kupanda, basi tusiomboleze kwani utajiri si wa milele (Poor man mourn the rich riches increase. Be not grieved, riches are not forever )
Huu ni kati ya nyimbo zilizo na UJUMBE NA HISIA KALI saaana toka kwa Buju na ambao una "tempo" inayoendana na ujumbe wake. Naamini kwa kuusikiliza na kuusoma vema, kisha kushirikisha ujumbe kwa wenye uhitaji wasioweza kufikiwa na jumbe za njia hii, tutaweza kufanikisha kazi tuliyonayo ambayo ni kuwa na jamii kwa ajili ya jamii.
Msikilize Buju ukimsoma na kutafakari.

Intro...
one more day in the struggle
have to get up and juggle
yu done know
want a little sugar inna de pan
me nah see fi trouble no man

oh oh oh .....

Chorus
said I had close one yesterday
JAH put an angel over me, be strong
hold a firm meditation
one day things must get better
dont you go down
keep your head above the water
say, one day things must get better,
be strong
hold a firm meditation
one day things must get better
dont you go down
keep your head above the water
say, one day things must get better, be strong

Verse 1
the rich is wise in his conceit
but the fool with overstanding search him out
poor man mourn the rich riches increase
be not grieved riches are not forever
envy not the opressor choses none of his ways
be not wise in his own eyes
only jah you must praise
strive not with a man without cause
if he have done no harm
let by gone be by gone

Repeat Chorus

Verse 2
this nine to five is a joke
compare to the pressure
the minister say
the economy is getting better
misleading the people
the mass still suffer on jah
scarce benefit and spoils
jah know that we feel it
day**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa yote na IJUMAA NJEMA NAWE NA PIA FAMILIA YAKO.