Saturday, November 14, 2009

Happy Birthdate Brother Fadhy

Enzi zake.
Labda tuna sababu tofauti za ku-blog. Na huu ndio UKWELI. Na sitasema lolote kuhusu yeyote zaidi yangu.
Kwangu ku-blog kumekuwa KUISHI. Ni sehemu ya maisha na ninajiona kama mwana-FAMILIA kwenye ulimwengu huu. Nimejuana na wengi toka sehemu nyingi ULIMWENGUNI na kujuana huku kunaniwezesha kushirikiana na wengi.
Niseme nimekuwa na maRAFIKI wengi sasa na naweza kujua na kujuvya mwngi yanayoendelea ulimwenguni.
Na mmoja wa wale niwaheshimuo saana kwa kazi na mawasiliano ni Kakangu Fadhy Mtanga. Ambaye leo hii anatimiza mwaka mwingine kamili katika mzunguko wa maisha yake.
Sina ninaloweza kumueleza Kakangu huyu yakamaliza kila nililo nalo juu yake. Ntasema machache na kuzidi KUMUOMBEA.
Fadhy: umekuwa kiungo muhimu kwetu hasa kwa yale yatokeayo nyanda ulizopo. Pia mafunzo kwa LUGHA FASAHA ya kiswahili unapotuelimisha ukituburudisha kwa mashairi katika kukumbuka siku zetu, kusherehekea za wenzetu na hata kutafakari hili na lile.
Kwa ujumla NAKUHESHIMU NA NAKUOMBEA MAFANIKIO KATIKA KILA JEMA UTENDALO.
Endelea kuwa RAFIKI mwema ambaye tunaweza kujisikia wepezi wa kuja kukulia matatizo na magumu yetu kwani huo ni mmoja kati ya wajibu wa rafiki.
Umekuwa RAFIKI MWEMA na naamini utaendelea kuwa hivyo
Unapokumbuka siku yako ya kuzaliwa, nakurejesha katika wajibu wetu wa uRAFIKI kwa wimbo wake Beres Hammond uitwao Friends.
HAPPY BIRTHDATE BROTHER

8 comments:

Halil Mnzava said...

Hapo umeongea brother,naamini uliyomwombea MOLA atayapokea.
Wasalam!

Yasinta Ngonyani said...

Mungu akujalie uwe na afya na uzima. HONGERA kwa siku hii mtani.

John Mwaipopo said...

hongera kwa kuongeza miaka ya kuishi hapa duniani. mti uliopandwa leo (pengine na wewe au kokote kule) ukue na utakapotoa matunda yake kwa mwaka wa 100 basi moja ya matunda hayo liliwe na wewe.

Mija Shija Sayi said...

Hongera brother Fadhy.

PASSION4FASHION.TZ said...

Happy birthday kaka Mtanga.

chib said...

Natumaini Fadhy amekupata. ongera zake

Masangu said...

Happy birthday to you, happy birthday to you...sijui wimbo huu unavyoendelea huko mbele lakini nadhani ujumbe umemfikia MALENGA!

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana kaka. Ni miaka 8 tangu unitakie heri humu;ni kama juzi tu.