Tuesday, November 24, 2009

Hongera wana-STRICTLY GOSPEL

Kwa muda sasa tumekuwa tukijaribu kupiga hatua ya ziada kwenye uhabarishaji na uelimishaji wetu kuwagusa wengi wahitajio lakini hawana namna ya kupata habari ihizi kupitia mtandao. Tumejadili kuhusu kuweka makala na maandishi yetu kwenye MAGAZETI na MAJARIDA na bado naamini tutafanikisha jambo hili ili tuweze kuwafikia wengi zaidi.
Kwa sasa niwapongeze wanaSTRICTLY GOSPEL kwa kufanikiwa kuvuka kizingiti hiki kwa kuweza kuanza kuchapisha jarida lao liendalo kwa jina hilohilo.

Wamesonga hatua moja mbele kutoka wana-mtandao pekee (blog) mpaka mtandao na jarida.
JIANDAE KUPATA NAKALA YA JARIDA HILI HIVI KARIBUNI

8 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nilikuwa nafuatilia mjadala wako na John Paul na "wakereketwa" wengine wa blogu hiyo. Kama kawaida nadhani mjadala huo haukuisha kwani kuna watu ambao walikuja juu na kutaka usitishwe.

Hii ni hatua nzuri na hasa kwa Tanzania ambako kusema kweli bado watu wengi hawana huduma za mtandao. Japo kwingineko watu wanahamishia majarida yao mtandaoni ili kuepuka gharama na kuweza kufikia wasomaji wengi, sisi kidogo bado. Hii ni hatua nzuri na wanastahili pongezi. Mungu Aendelee kuwabariki.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaa. Asante kwa kufuatilia Kaka Masangu. Mjadala ULIFUNGWA wala haukuisha. Na hii ni kwa kuwa Kaka John aliamua kusitisha na kusema asingeendelea kuandika kujibu baadhi ya maswali yangu. (Fuatilia "sehemu ya mwisho" ya maoni hapa http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/21/dini-imani-na-wokovu-ni-vitu-gani/#comments)
Hivyo ni kweli kuwa HAUKUISHA KAMA NILIVYOTARAJI lakini pia HAUKUISHA KAMA AMBAVYO SIKUWA NATAKA. Ina maana licha ya kutoisha nisivyotarajia, hatukutokea kukwaza na Ndg John Paul kitu ambacho naamini ni chema.
Ninachofanya ni kuwasiliana na wanaStrictly Gospel ili nikienda nyumbani nipate kukutanishwa na Ndg John Paul kwani anaonekana ana mengi ya kushiriki nami na naamini nina mengi pia kwake.
Lakini naendelea kujifunza kwao na NAJIVUNIA MAFANIKIO YAO
Baraka kwako, kwa familia na wote wenye mapenzi mema nawe

Fadhy Mtanga said...

Nafurahi kuona ulimwengu wa kublog unachukua hatua nyingine. Ni hatua ya kupongezwa sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui kama wana jipya sana. hawa jamaa kia nikikoment kwao wananibania, comments zangu zinasitishwaga tu!!!!!!!!!!

sasa wametoa kitu, ni mafanikio lakini kwa uzoefu wangu nikwamba, machapisho mengi ya kikristo yananukuu bilblia na hivyo ni bora kusoma biblia zaidi. harafu gharama sijui shs ngapi

twenty 4 seven said...

big up...

Mzee wa Changamoto said...

Kamala!! Kwa mujibu wa gharama iliyoandikwa kwenye kurasa wa juu wa jarida ni shilingi 5000.
Nadhani na "yaliyomo" inayoonekana hapo, kutakuwa na habari mchanganyiko labda ila kwa kuwa ni la kirogo, basi naamini watakuwa waki"rejea" mistari na maandishi ya kitabu kitakatifu.
Nasubiri litoke nisome na kuona.
Ukisoma kabla yangu nijuvye pia.
Blessings

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Mzee wa C/moto, sidhani kama kweli nitaweza kusoma jarida hili na sifikirii sana kulisoma! kitabu kitakatifu ni kipi hicho?

siwezi kutumia muda wangu kusoma dogma yaani majarida ambayo yanazuia baadhi ya maoni kwani naamini katika uhuru wa maoni.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kamala - hawa huwa hawatoi maoni ambayo yanapingana au kuhoji "ulokole" Mimi pia niliwahi kuuliza jambo la msingi sana ambalo limenitatanisha kwa muda mrefu pamoja na kusoma vitabu kibao. Comment hiyo haikutoka. Siku hizi nikiweka comment huko basi ni lazima iwe ya "Bwana Asifiwe" Ndiyo maana nilishangaa kidogo nilipoona maswali "makali" aliyokuwa akiuliza Mzee wa Changamoto yalikuwa yakitoka. Pengine ndiyo maana wanajiita "Strictly Gospel" na wewe kama unauliza maswali ya kiduniadunia basi wanakutupa kapuni.

Mzee wa Changamoto nakubaliana nawe kuhusu Ndugu John Paul. Ni mtu ambaye, kama wewe, ana welewa mpana sana wa masuala mbalimbali na ndiyo maana mjadala wenu ulikuwa makini na wa kuvutia. Ilikuwa ni bandika bandua ya hoja kwa hoja. Uchambuzi wake mara nyingi huwa ni wa kina bila kujali kama unakubaliana naye ama la. Siku hizi nikiwa na maswali namwandikia yeye moja kwa moja.