Saturday, November 7, 2009

Mmmmhh!! Hii kali.. Mko mazikoni na jeneza lenye maiti kisha "marehemu" anaungana nanyi kuzika.....

Huko Brazil kumetokea "kisanga" ambapo mwanaume mmoja amejikuta akihudhuria kile kilichodhaniwa kuwa ni MAZISHI YAKE. Ademir Jorge Goncalves alidhaniwa kuwa amefariki kwenye ajali ya gari iliyotokea kusini mwa eneo la Parana ilhali alikuwa na rafikize wakinywa pombe usiku mzima. Katika ajali hiyo, mtu mmoja ambaye alikuwa na nguo zifananazo na za Ademir aliharibika vibaya kiasi cha kuwa vigumu kumtambua, hivyo ndugu za Ademir waliuchukua mwili na kuanza taratibu za mazishi japo mama yake mzazi alipoangalia mwili huo aliutilia shaka.
Soma habari kamili HAPA
Na huko Pennsylvania kijana Cesar Lopez anayekadiriwa kuwa na miaka 29 alificha bangi yake kwenye kofia, lakini bahati mbaya alikuwa ametoka jasho na ki-pakiti hicho cha bangi kikatoka kwenye kofia na kunasa kwenye paji la uso bila yeye kujua. Kisha akaingia kwenye duka moja na kutoa kofia kukitafuta (sijui kwa nia ya kuuza ama kugawa) na wakati anakitafuta, polisi aliyekuwa pembeni yake akakiona kikiwa kimenasa kwenye PAJI la uso. Kwa ukarimu kabisa, Polizi huyi akakibandua kisha akamuweka chini ya ulinzi.
Sijui aliwaza nini kutafuta BANGI yake mbele ya Polisi?????
Soma habari kamili BOFYA HAPA

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mikasa ya maisha hii. Ni kama ule wa juzi ambapo Meja wa jeshi aliamua kuwamiminia risasi wanajeshi wenzake katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood kule Texas. Ndiyo dunia yetu hii - imejaa kila aina ya misukosuko na mikasa, mingine ya kufurahisha, mingine ya kusikitisha ali mradi ni mvurugano mtindo mmoja; na kwa kuwa tupo (japo hatukuchagua kuwepo) basi ni lazima tupambane nayo!

Huyo jamaa aliyehudhuria mazishi yake mwenyewe natumaini ataishi maisha ya kiadilifu kuanzia sasa kwani ameshaona zamu yake mwenyewe "ikiahirishwa". Huyo mwenye bangi nadhani alikuwa ameshaonja msokoto tayari...

Faith S Hilary said...

Duniani kuna mambo

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmhhh! kazi kwelikweli kweli duniani kuna mambo tena makubwa tu