Tuesday, December 1, 2009

Kutokomeza UKIMWI...........YES WE CAN!!!


Pengine yaweza kuonekana kama ndoto, na pengine yaweza kuonekana kama ni kitu kisichowezekana, lakini kwa hakika ni jambo linalowezekana. NAZUNGUMZIA KUTOKOMEZA UKIMWI NCHINI NA DUNIANI.
Japo ni kitu kiwezekanacho, lakini chahitaji jitihada za ziada. Twahidaji malengo na pia utekelezaji wa nia. Twahitaji kubadilika na kuacha kufanya ugonjwa huu kama mradi. Kisha kwa pamoja kuungana na walioathirika katika harakati zao za kuwa wazi. Wakiacha kunyanyapaliwa, wakapendwa, kuheshimika na kukubalika ndani ya jamii, watakuwa wazi zaidi kueleza namna tofauti walizopitia kufikia hali hiyo na kwa kufanya hivyo tutaepusha maambukizi mapya na kurefusha maisha ya wale wenye virusi hivyo. Japo idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huu vimeonekana kupungua kwa mwaka 2007 kwa mujibu wa TAKWIMU ZA W.H.O, bado tuna kazi ya ziada kuhakikisha tunawezesha namba ama takwimu hizi kufikia sifuri, yaani kuutokomeza ugonjwa huu.
Na hii ni CHANGAMOTO YETU sote.
Kuutokomeza ugonjwa huu wa UKIMWI...... NDIO TWAWEZA
Tumwangalie dada huyu alivyoelezea namna alivyopokea matokeo ya vipimo vyake. Amekuwa muwazi juu ya hali yake, amekuwa mwelimishaji na mwanaharakati mwema kuhusu ugonjwa huuVideo yake kamilifu kuhusu biashara mbaya ya kuuza mwili pale UWANJA WA FISI waweza kuipata kwa kutembelea http://www.hyenasquare.org/
Basi tusikie wasanii nyota wa Uganda wanavyoungana kwenye mapambano haya muhimu juu ya gonjwa hili hatari.
"A little bit LOVE,
A little bit HOPE
A little bit CAUTIONA IS ALL WE NEED
A little bit WISER
A little bit SMARTER"


Ama twende CONGO ambako nao pia waliungana na kutoa kibao hiki kuhusu ugonjwa huu wa UKIMWI

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu " Kisha kwa pamoja kuungana na walioathirika katika harakati zao za kuwa wazi. Wakiacha kunyanyapaliwa, wakapendwa, kuheshimika na kukubalika ndani ya jamii, watakuwa wazi zaidi kueleza namna tofauti walizopitia kufikia hali hiyo na kwa kufanya hivyo tutaepusha maambukizi mapya na kurefusha maisha ya wale wenye virusi hivyo." mwisho wa kunukuu:- Hapa nakubaliana kabisa kwa sababu kuna wengine wakisikia tu fulani ana ukimwi basi hwataki hata kumsalimia kwa kuogopa kuambukizwa. Sababu hawajaelimishwa ni vipi unaweza kuambukizwa. Na pia wengine kama ulivyosema wanafanya ni biashara kabisa kwa nini mimi tu basi anasambaza kijiji kizima. Juzi nilipokuwa nyumbani nilikuwa nimeenda kusuka ilikuwa ni njiani tu kwa hawa wamasai. Na mara akapita mama mmoja nikasikia wamasai wanasema eeh bwana angalia yule mama kanenepa mpaka namtamani tena yaani anaonekana kama kawaida lakini kaathirika huyu. Ila Duh! nilisikitika sana. Na kwa kweli inasikitisha sana. Ahsante kwa hiyo video ya fisi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kama ukiangalia vizuri kinachoendelea ulimwenguni, utagundua kuwa huu ndio mwisho wa ukimwi na sasa yanazuka magonjwa mengine kama mafua ya kuku, nguruwe nk. muda mfupi watatuletea dawa