Monday, December 7, 2009

Nina-blog kujifunza

Kwa mara nyingine napenda kutumia maoni ya Kakangu Kamala kujibu hili swali la Kaka Matondo juu ya ku-blog.
Labda sikuanzisha nikitegemea kujifunza kwa kiwango nijifunzacho sasa, lakini nilijua kuwa kwa kuruhusu Maoni ningepata changamoto na mawazo mengi mapya kuhusu mambo mbalimbali niandikayo.
Sasa nimeona niwashirikishe maoni haya ya Kamala kuhusu swali langu hapo chini kuhusu JAMII inavyokuwa baada ya kuchagua na kuchaguliwa. Yaani tunavyotegemea kuchuma tusipowekeza na wale wanaochuma ambapo walikuwa wakipashutumu.
Msome mwenyewe hapa chini.....
KUMBUKA...Toleo lilisema KABLA YA KUWA WAO, WANAKUWA SISI....NI SISI WA KUBADILIKA.

Kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nimeona mengi kwa kuchunguza. vijana walioko vyuoni wanailalamikia serikali na kuona kila uoza harafu baadaye wanaingia serikalini nakuwalalamikia wanaoilalamikia serikali.

kwa mfano kuna yule mwandishi wa rais Salva Rweyemamu, alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali na upuuzi kibao, baada ya kupewa nafasi ikulu akawa wa kwanza kuyafungia magazeti yenye mitizamo kama aliyoyaandikia yeye (Mwanahalisi) kwa hiyo wale wanaoilalamikia serikali wanawaonea wivu na wale walioko serikalini wanafurahia ulaji. ndio maana wanasiasa wetu hushukuru baada yakuchaguliwa badala ya kutafakari kazi ngumu baada yakuchaguliwa.

au ndio maana watu huonga ili wachaguliwe nawengine huongwa. tatizo ni refu. ndio maana tukienda vijijini hujitenga na jamii ile hatusaidii kufanya lolote.

nilikuwa kijijini kwetu, pitapita yangu unakuta watu wamejenga majumba makubwa yakifahali na ya gharama kuubwa vijijini, harafu wanaendaga mara moja tu kwa mwaka au mara moja kwa miaka miwili na kukaa siku mbili au wakati mwingine hulala hotelini mijini. kajenga nyumba ya gharama na anatumia gharama kuitunza harafu hainafaida, jirani wanakaa kwenye mbavu za mbwa harafu shule aliyoisomea haiana madawati, majengo ya udongo.

yaani badala ya kujenga nyumba yakawaida tu napesa nyingine tuipeleke kujenga shule, zahanati au huduma nyingine za jamii, tunajijengea nyumba tusizohitaji.

tukienda vijijini tunanunua pombe na kulewesha watu badala ya kuchangia vitu vya msingi. Harusi, natarajia kufunga yangu naninaonekana kichaa na chizi kwa kukwepa kuchangiwa mamilioni. tunachangia maharusi huku tukiwa na bara bara mbovu, mitaro mibovu nk, nk

hatutaki kurudi vijijini kusaidiana na kuelmisha na wananchi, sisi ni wakazi wa tauni na kazi kuubwa ni starehe.

kama tunataka mapinduzi tuanze na yale ya kifikra. namshukulu sana Munga tehenan kwa kujitolea kunipa maarifa ya utambuzi. ni maarifa ya gharama sana nchini marekani na masikini hawezi yapata kwani bei iko juu. Munga aliyatafuta kwa gharama na kuyapata kwa shida ila akatugawia bure na kutubadilisha, aliona fedha haina maana sana. huo ndio mfano wa kuigwa wa kubadili jamii na sio kusubili tupate nafasi za uongozi wakati sisi tayari ni viongozi

naishia hapa ila mimi, wewe, yule tuanze leo kujirekebisha sisi na wengine watarekebika tu "change yourself so that you can change the world"... Sant baljit Singh

Monday, 07 December, 2009

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mubelwa, nilisoma maoni ya kaka Kamala. Ni maoni yanayofikirisha sana. Ni maoni yenye nguvu. Ameeleza ukweli mtupu. Na ndivyo ilivyo.
Natamani kuiona jamii yenye kutetea kweli na haki pasipo kujali madaraka wala uwezo kimamlaka. Lakini kwanini binadamu hubadilika na kuziasi imani zao na itikadi za 'kabla'
Kaka Kamala umesema yote.