Friday, December 4, 2009

Them, I & Them....NOTHING TO SMILE ABOUT.....Morgan Heritage

Hii ni ijumaa ya mwisho kabla nchi yangu haijatimiza miaka 48 tangu ipate uhuru. Wow!!! 48. Ni karibu nusu karne sasa. Na TUMEBARIKIWA mengi. Amani, Maliasili, Watu, Ardhi japo sijajua kuhusu SIASA SAFI.
Ukiwa unafanya utafiti kuhusu Tanzania utapenda utakayoyasoma humo. Nchi ILIYOBARIKIWA kuwa na mbuga, madini, vyanzo vingi vya maji (yangetumika kwa matumizi ya nyumbani, kilimo na uzalishaji wa umeme), hali ya hewa inayowezesha ukulima, udongo wenye rutuba na mengine mengi.
Lakini ukishatua nchini (na zaidi vijijini) ndipo unapoweza kuona tofauti ya takwimu na hali halisi ya maisha. Kama walivyosema Morgan Heritage kuwa kwa watalii, nchi zetu ni "PARADISE, but for those who were born, raised and living there, it's a STRUGGLE". HAKUNA LA KUKUFANYA UTABASAMU UINGIAPO VIJIJINI ambako ndiko kwenye watu wengi.
Hawajaliwi, hawawekezewi, hawawezeshwi, hawakumbukwi na licha ya HOTUBA NA AHADI nyingi toka kwa WATAWALA, bado nchi yetu inazidi kusonga umaskinini kwa kasi ya ajabu.
Ni ukweli usipopingika kuwa WATAWALA wetu wameshindwa KUWATUMIKIA WANANCHI na KUFANYA KILA LILILO KATIKA UWEZO WAO KUWAONDOLEA WANANCHI KERO WASIZOSTAHILI.
Sina hakika kama HOTUBA ya Rais siku ya UHURU imekamilika, lakini kama bado anaandika ningependa kumueleza kuwa MWANANCHI MIMI napenda kusikia majibu ya maswali kadhaa niyapatayo niangaliapo taswira zifuatazo.
Labda swali ni kuwa MIAKA 48 baada ya uhuru, ni kwanini tunaona taswira tuonazo hapo chini katika nchi iliyokuwa na AMANI miaka yote na yenye MALIASILI NYIIIINGI namna hii?
Na pia atuambie kuwa ANAFANYA NINI KUONDOA HILI?
Mheshimiwa Rais, wanaoisifia Tanzania kwa kuisoma kwenye Takwimu mnazobandika wanatuumiza zaidi sisi tuijuao kwani kila tukitembea nchini hatuoni la kutufanya tujivunie.
For sure there's NOTHING TO SMILE ABOUT.
Na hizi hapa chini ni taswira zilizobandikwa ktk blog hii kwa miezi 15 ilyopita ambazo zaonesha maisha na uhitaji wa waTanzania wengi. Ni ndani ya miaka 48 ya UHURU. I hope Raisi atagusia (japo moja kati ya) haya kwenye HOTUBA YAKE
ELIMU ya kutuletea wanazuoni wa keshoBweni la sekondariWodi ya kinamamaWawekezaji wao na kemikali kwenye vyanzo vya maji yetu (sio yao)Mitaani kweti kina sie"DO YOU SEE ANYTHING TO SMILE ABOUT?"


Lyrics za wimbo na maelezo viko HAPA
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
PICHA ZILITOKA BLOGU MBALIMBALI....ASANTENI

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli inasikitisha na hakuna la kumfanya mtu atabasamu. Miaka 48 ya uhuru, KWELI TUPO HURU? sijui kwa kweli. Upendo daima na Ijumaa njema pia

Halil Mnzava said...

Nimetabasamu si kwa kufurahi, bali kwa masikitiko.
Kisha nikapata swali je wenye dhamana wanajali hali hizi?

Mbele said...

Masuala haya ni magumu. Vyanzo vyake ni vingi na utatuzi wake utahitaji mikakati mingi.

Elimu duni inachangia. Kwa mfano, kwa nini watu watupe takataka ovyo. Hata wakiwekewa mapipa ya kukusanyia takataka, wanatupa takataka kila mahali. Imefikia mahali hata bustani ya Mnazi Mmoja imefungwa. Tatizo ni wananchi, sio watawala.

Wananchi hao wanaposafiri ndani ya basi kwenda mikoani au kutoka mikoani, wananunua viplastiki vya karanga na wakishatafuna hizo karanga wanavitupa viplastiki hovyo nje ya madirisha. Vyupa vya vya plastiki wanavitupa hivyo hivyo. Pembeni mwa barabara hizo kuna takataka hizo ambazo zinaathiri mazingira. Tatizo ni wananchi, si watawala.

Kwenye baadhi ya hizo picha, tunaona vijumba ambavyo kuta zake ni ovyo kabisa, ingawa ni kuta za udongo. Udongo haununuliwi; uko hapo hapo pembeni ya nyumba. Ni kiasi cha kuchukua jembe na maji na kurekebisha hizo kuta. Huu uzembe ni wananchi, si watawala. Hayo mapaa ya nyasi yaliyokaa ovyo ni uzembe wa wananchi. Karibu kila mahali Tanzania miti na nyasi ni rahisi kupatikana. Wananchi wangeweza kukarabati hizo paa za nyasi.

Sisi wenye uwezo kiasi, tunaoishi Dar, Arusha, Mwanza, au majuu, tukishaona hali hiyo inayoonekana kwenye baadhi ya picha, kwa mfano hizi shule, hatuchangi hela za kununulia madawati. Tunaenda kwenye vikao vya arusi na kuchanga sh. 50,000 au zaidi kufanikisha arusi.

Hapa Marekani waTanzania wanasafiri masafa marefu kuhudhuria sherehe Columbus, Houston, Atlanta, Washington DC, na kadhalika, kwa gharama kubwa, badala ya kutuma hela hizo kwenye hivi vishule vinavyoonekana pichani, vikanunue madawati na vitabu.

Wakati waTanzania wanaendekeza matanuzi, utawaona waMarekani wanajituma kwenda kwenye vijiji vyetu kujenga au kukarabati mashule, kuchimba visima na kuweka mabomba ya maji, na hata kuchangia ada na matumizi kwa wanafunzi.

Hapa Minnesota, kwa mfano, wakati sisi waTanzania tunasherehe zetu kwenye Boat Party, waMarekani wana miradi kama Saint Paul Partners, ambayo ni ya kushughulikia maji mkoani Iringa. Wana mradi wa Bega kwa Bega, ambao unashughulikia maendeleo ya shule na kadhalika kule kule Iringa. Wengi wanasafiri kwenda kule na kuchangia maendeleo haya, au wanatuma fedha.

Wanajitolea vihela vyao, hata wakati huu wa uchumi mgumu, wakati sisi waTanzania tulioko pale pale mkoani, Dar es Salaam, au majuu, tunaendelea na makamuzi.

Wamarekani wengi, watu wa Canada na Ulaya wako vijijini Tanzania wakifanya shughuli za kujitolea, wakati wananchi wenyewe wenye kipato wako baa wanakamua, au wanapita barabarani wakiwa na magari ya fahari.

Watawala wetu wana matatizo makubwa. Ni kweli. Lakini sisi wenyewe ni sehemu ya tatizo. Na tatizo letu jingine ni kuwa tunatafuta mchawi, yaani serikali, hata pale ambapo wachawi ni sisi wenyewe wananchi.

Miaka 48 ya Uhuru imepita, lakini vichwani mwetu wananchi na vichwani mwa viongozi wetu, Uhuru huo haujaingia.

Serina said...

DUH!!!

Nothing to smile about!

Mzee wa Changamoto said...

Wow!!
Asanteni nyote kwa maoni.
Kwako Profesa. Ulilosema ndilo nililowahi kuuliza Dec 27 mwaka jana nilipoandika "Ni kama hadithi ya kuku na yai" (http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/12/ni-kama-hadithi-ya-kuku-na-yai.html) ambapo niliuliza wanapojenga mabondeni na kuwekewa umeme kisha wakahamishwa ni nani wa kulaumiwa? Viongozi wanaziona taka zinapoanza kurushwa na kurndikwa lakini HAWATIMIZI WAJIBU WAO KUKEMEA. Jamii yetu ina watu ambao wanafurahia kwenda against utaratibu.
Wanaona watu wanajenga mabondeni hawasemi mpaka miaka kadhaa wanapitisha bomoa bomoa na kuwalipa ilhali hawakustahili hata kulipwa.
Wanaona wananchi wao wana familia lakini hawana vyoo na wanakaa kimya, kipindupindu kikifumuka wanaathirika hata wasio na hatia.
Kuna wajibu unaokwepwa nasi sote lakini naamini viongozi wana wajibu wa kuwasukuma wale wazembe kutimiza hayo. Nina hakika ni asilimia ndogo saana ya watupa taka hovyo ilikuwepo miaka 10 iliyopita, lakini kwa kuwa haikukemewa, sasa hivi yawezekana ni mara mbili yake na watoto waliozaliwa na kukua wakiona hilo, wanaona ni MFUMO WA MAISHA.
Bado najiuliza ni nani wa kubeba lawama kiasi gani katika uozo huu unaonekana hapa?
Nakumbuka wakati Phillip Mangula akiwa mkuu wa mkoa Kagera alikuwa na standard ya vitu. Kama ni kitu kisicho na gharama (kama ulivyosema kuhusu nyumba) ungeitengeneza tuu ama ungekumbana na urekebishaji wake.
Kama mzazi asipompeleka mtoto shule anashitakiwa (kwa kuwa shule ni bure) kwanini asipokandika nyumba yake asishitakiwe (kwani udongo ni bure na asipoikandika anahatarisha maisha ya watoto?)
Nakubaliana nawe kuwa WANANCHI WANA MAKOSA, lakini wajibu wa kiongozi ni kuhimiza, kusimamia na hata kushurutisha maendeleo ambayo ni ya lazima.
Na ndio maana kuna wakati niiliandika "Dikteta ni nani na kwanini twamhitaji? (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/dikteta-ni-nani-na-kwanini-twamhitaji.html)
NAJIFUNZA MEEENGI TOKA KWENU
ASANTENI

Mbele said...

Mzee wa Changamoto, haya masuali yako ya ziada naona yana nguvu sana, na yanatufikisha mbele zaidi kwenye tafakari ya hili suala tata.

Mija Shija Sayi said...

Kosa bado ni la viongozi.

Hivi nikuulize mzee wetu wa changamoto, Paulina atakapokosa adabu hapo baadaye atakayelaumiwa kwanza ni nani?... watu wataanza kuangalia kwanza umemlealeaje hadi kafikia tabia hiyo mbovu, baada ya hapo wakikuta huna kosa ndo watamlaumu mtoto.

Sasa kwa nchi yetu, viongozi ambao ndo wazazi wetu wanatudekeza mno, wanatuachia tufanye tunalotaka mf, hayo ya kujiwajibikia wenyewe kama kutupa taka hovyo, kutokwenda shule, kutokujenga nyufa za nyumba zetu n.k... ni kwa nini hawatuchukuli hatua madhubuti?

Mzee wa changamoto mbona huku ulaya hatufanyi ujinga? mbona hatutupi taka kila mahali, unakuta eneo lenu mapazia ni lazima yafanane kwa nje mbona tunafuata? Ni kwa sababu wazazi ni wakali na ndo maana mambo yanaenda sawa.

WATANZANIA BILA UDIKTETA NI NGUMU.

Ni hayo tu, naomba kuwasilisha.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nadhani tatizo liko kwa wananchi kuliko vingozi kwani viongozi ni sehemu ya wananchi. tutachagua tena kutoka kwa wananchi kuwa viongozi na wanaochagua ni wananchi sio viongozi harafu kikawaida sis sote ni viongozi tatizo tunasubilia kuongozwa badaa ya kujiongoza harafu tumekuwa wapigadomo wa kutafua mtwishwa lawama badala ya kucheza naasi yetu.

naamini tukiamua sisi wenyewe hata sisi bloggers tunaweza kubadilisha hali na kuleta ahueni pahala na kubadilisha mambo na kufanya jambo jipya tunalolihitaji badala ya kuwa lalamikia watu fulani

Albert G.Sengo said...

Yote haya yanafanyika wazi wazi tena bila kificho tatizo sasa wakemeaji wakuu wanaogopa kukemea wakilinda maslahi yao kisiasa. Tunayo safari nayo si yakitoto.

Albert G.Sengo said...

Yote haya yanafanyika wazi wazi tena bila kificho tatizo sasa wakemeaji wakuu wanaogopa kukemea wakilinda maslahi yao kisiasa. Tunayo safari nayo si yakitoto.