Monday, January 25, 2010

ADIMIKO

Image from Metal Blades Logos
Kutokana na kupanga na kufuatilia masuala fulani ya mustakabali wa maisha, nategemea kuadimika kwa muda hapa. Haimaanishi kuwa sitakuwa naweka mabandiko, na si kwamba sitakuwepo kwa muda mrefu. Nitakuwa nikishughulikia mambo mengi na hivyo naweza kutokuwa na wakati wa kutosha kutazama mambo kwa "jicho la ndani" kuniwezesha kuyabandika hapa.
Najua ntapata nafasi ya kupitia "sebule" za wapendwa na pale niwezapo kuacha maoni yangu kwani hiyo ni SEHEMU YA RATIBA YA KILA SIKU
Kwa wakati huu wa u-adimiko langu, endelea kuwa salama, mwenye furaha na amani ndani na mazingirani mwako

UPENDO KWAKO

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa taarifa. Hivi ndivyo inavyotakia KUTOA TAARIFA:-) Kila la kheri

Mija Shija Sayi said...

Kila la heri kaka tupo pamoja.

Halil Mnzava said...

Tuombeane uzima.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

byee

Simon Kitururu said...

Upendo kwako pia Mkuu! Tuko pamoja!

Jeff Msangi said...

Asante kwa taarifa.Inaeleweka kabisa kwamba kuna wakati mtu inabidi ukimbie kidogo kutoka bloguni ili kuweka sawa mambo mengine.Kila la kheri

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Naamini kwamba unaadimika sasa ili uje upatikane huko mbele. Kwa hiyo yote ni sawa. Tutakusubiri!