Sunday, January 31, 2010

Ya Dada Koero na Kaka Matondo yatimia

Januari 22, Da Mdogo Koero binti Mkundi aliandika kuhusu RAISI AMANI KARUME NA MKAKATI WA MARIDHIANO (Isome hapa)ambapo alichanganua kinaga ubaga kuhusu KIINI MACHO kinachoendelea Zanzibar. Yakaja maoni mengi na wengi walionekana "kushitukia" kinachotengenezwa kisiwani humo. Lakini Kakangu Mwalimu Matondo alitoa maoni na AKAONYA kuwa "Kamwe usimwamini mwanasiasa hata kama ni baba yako, mama yako, mke wako au mtoto wako.
Kamwe usimwamini mwanasiasa - HATA KAMA NI WEWE MWENYEWE!"

Hii ni baada ya kutukumbusha kuhusu "mchezo mchafu upumbazao" unaoendelea kwenye siasa aliouandika HAPA
Sasa jana tumesikia KUPITISHWA KWA SERIALI YA MSETO ZANZIBAR.
Hakuna ambaye anapinga kupatikana kwa SULUHU ZANZIBAR japo hakuna mwenye akili timamu ambaye hatasita kuwaza
1: kwanini sasa?
2: Kimebadilika nini leo ambacho hakikuwepo miaka iliyopita?
3: Ni nani aliyekwamisha hayo mabadiliko?
4: Ni nini kitatokea kwa ambaye alisababisha kutotokea kwa mabadiliko yalisababisha "mafanikio" ya sasa?
Na swali langu binafsi ni kuwa "kama wote walioshiriki kuipata serikali ya mseto wakiambiwa wamefanikisha HATUA KUBWA YA KISIASA NCHINI ZANZIBAR HIVYO WAPUMZIKE watakubali ama hii ni kujisafishia njia kuelekea uchaguzi?
Habari kamili ya maridhiano hayo iko
HAPA KWENYE GAZETI LA MWANANCHI

Morgan Heritage waliwahi kuuliza
"why should we trust politicians and why should we vote every election? When there's no place for we, you and me. In their secret society they call us minority."

Wasikilize hapa chini.Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sipendi saana poll trics, ila wameona hawatashinda, wakaongea na Maalimu wakamuhaidi vyeo yeye na wenzake, sasa wanatekeleza

Koero Mkundi said...

Nafurahi kuona kuwa kile nilichosema kinaanza kudhihiri, na bado tutashuhudua mengi, huu ni Mwanzo tu

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Niliposema "Kamwe usimwamini mwanasiasa hata kama ni baba yako, mama yako, mke wako au mtoto wako.
Kamwe usimwamini mwanasiasa - HATA KAMA NI WEWE MWENYEWE!" nilitaka kusema kwamba pengine KILA MMOJA wetu ana uanasiasa fulani ndanimwe. Hivi ni nani ambaye hajatoa ahadi akashindwa kuitimiza? Ni mangapi tunayosema lakini hatuyatendi?

Hivi karibuni Kamala alileta ombi hapa la kutaka kumsomesha kijana Nestory anayesoma kwa shida sana. Wanablogu wengi tumepiga makelele sana kulaumu tabia yetu ya kupenda kuchangia mambo ya starehe kama harusi na kitchen party na kupuuza mambo ya msingi kama elimu. Ningetegemea kwamba tungeliitikia ombi hili la Kamala kwa moyo mmoja. Habari nilizonazo hata hivyo ni kwamba ombi hilo halikuitikiwa vizuri. Sasa hapo mwanasiasa ni nani?

Naona sote ni wanasiasa tu!