Tuesday, February 9, 2010

Akutwa hai wiki nne baada ya tetemeko HAITI

Image from Daily Mail
Naliona hili kama TUKIO LA AJABU NA LA KIPEKEE.
Nasema kuwa NI AJABU LA KIPEKEE baada ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Evan Muncie mwenye umri wa miaka 28 ameopolewa katika kifusi ndani ya soko alimokuwa akifanya kazi kilichotakana na tetemeko la ardhi lililotokea wiki nne zilizopita. Hili limetokea zikiwa ni wiki 2 tangu kusitishwa kwa huduma za uopoaji.
Akizungumza na madaktari, Evans amesema alikuwa akiletewa maji na "mtu aliye katika mavazi meupe". Japo hakuna anayeweza kuthibitisha hili, lakini madaktari wamesema ni wazi kuwa asingeweza kuwa hai kama asingekunywa maji kwa muda wote huo. Wamesema angeweza kukaa bila kula (kama angepata maji) lakini wanahisi alikuwa na namna ya kupata maji ama kimiminika. Kakangu Dr Faustine ama Dada Subi na watabibu wengine wanaweza kutueleza uezekano wa kuishi muda huu wote bila kinywaji wala chakula ama bila kimojawapo.
Kupatikana kwa Evans siku zote hizi kumekuwa na ATHARI-CHANYA kwangu (na naamini kwa wengine wengi) lakini binafsi kumenifanya kujiuliza:
1: alikata tamaa mara ngapi kwa wiki nne alizokuwa amefunikwa na kifusi?
2: huyo asemekaye kumletea maji akiwa na vazi jeupe ni nani? Na hili lanirejesha katika MJADALA MZITO kuhusu kilichosababisha tetemeko la Haiti ULIOANZIA kwenye maoni ya mwisho mwisho HAPA kisha UKAHAMISHIWA HAPA ambapo wapo waliokuwa wakiamini kuwa kilichotokea Haiti ni ADHABU KWA KUABUDU DINI ZAO ZA ASILI.
Najiuliza kama huyo aliyesemwa kumletea maji mara kadhaa ambazo Evans alikuwa amenasa kwenye kifusi (kama ni kweli alikuwepo) ni Mungu (kama wengi wasemavyo) ama la?
Ninalojua ni kuwa kwa namna yoyote ile, kupatikana kwa Kaka Evans KUMEDHIHIRISHA KUWA KUNA NGUVU ZAIDI YETU na licha ya watu wengi kutokuwa na imani juu ya uwepo wa mtu yeyote akiwa hai takribani wiki mbili sasa, imekuja kudhihirika kuwa hawakuwa sahihi.
Kama nilivyofunzwa, IMANI NI KUWA NA HAKIKA YA MAMBO YATARAJIWAYO. BAYANA YA MAMBO YASIYOONEKANA.
Na kwa hili nasema Evans ALIKUWA NA IMANI, NASI TWAHITAJI IMANI.
Tazama ripoti ya Dr Sanjay Gupta wa CNN hapa chini

7 comments:

Fadhy Mtanga said...

Nikijaribu kulitazama jambo hili kwa macho ya kawaida naona ni jambo lisilowezekanika. Lakini kama ambavyo nawe umeona, yawezekana kuna nguvu kubwa juu yetu zaidi ya vile tuwezavyo kufikiria.
Dunia imejaa miujiza ambayo mara zote hutuachia maswali 'imewezekanaje?' ama 'imekuwajekuwaje?'
Huu kwangu nautazama kama muujiza. Kijana mwenyewe, namtazama kama mtu mwenye bahati ya kipekee zaidi.

Anonymous said...

Kama una imani za kidini, yote yawezekana kwake aliye tuumba. Mungu anatuthibitishia kuwa yupo hai. Silazima tuone malaika wanapeperuka angani kuamini miujiza ya Mungu, hii ndiyo miujiza yenyewe.

Simon Kitururu said...

Najiuliza tu KWANINI yeye?

Labda naye anajiuliza pia kwanini yeye wakati MTUZ kibao zimeanza?

Nasubiri kwa hamu siku akipona na kutoa maelezo yake mwenyewe.

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy:- Bahati si kweli ila tu alipofukiwa hapo alikuwa na imani kuwa siku moja atakuja kuokolewa na kweli ameokolewa. Imani yake, ucha mungu wake. IMANI!!

Mary Damian said...

Kaka Mubelwa! suala la muujiza na Imani elimu ya kidaktari haiwezi kitu...Mungu anaweza kufanya lolote maana yeye anajua yote!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui kwa nini faith unasema ni bahati, waliokufa hawana bahati? hivi kati ya kuishi na kufa, ipi ni bahati?

anony sijui imani za kidini??? sio kidini ila kinachohitajika ni imani, sio dini~

Yasinta labda uko sahihi juu yaimani yake hiyo na ni kweli inafanya kazi

juu yamtu mwenye mavazi meupe na mungu, labda lakini nigewashauri mtafute kitabu kiitwacho 'believe in miracles' cha path ya sanmat meditation muone miujiza zaidi ya hii ila kuna mengi yanayowezekana katika masuala ya meditation na kila jambo lina sababu yake kwanini asife nk

mengine ni masomo kwetu pia

chib said...

Kweli hii ni ajabu.
Nakiri ya kuwa kama alikuwa anapata maji kwa njia yoyote ile anaweza kuwa hai hadi muda huu, maana kuna watu waliweza kuishi aidi ya mwezi kwa kupata maji huku nguvu zikipukuchuliwa kutoka kwenye misuli na mafuta ya mwili.
Suala la huyo mtu mwenye mavazi meupe kumletea maji DUH! hiyo haielezeki kwa sayansi ya kawaida.
Mimi nafikiria ya kuwa humo sokoni alipofunikwa siku za mwanzo alijichana sana vyakula vilivyokuwepo, vilipoisha au kuharibika hapo sijui, labda mix ya mkojo nk.
Nakubaliana na Kitururu ya kwamba tusubiri akipata nafuu aongee vizuri, maana akili yake bado ina mshtuko na mauzauza kwa sasa.