Monday, March 22, 2010

Hongera kaka Fadhy na BLOGU YA "MWANANCHI MIMI"

Leo nasimama nikijivunia kushuhudia mabadiliko na maendeleo mengine kwenye ulimwengu huu wa ku-blog kwa Kiswahili. Ulimwengu ambao kama ilivyo kwa kitu chochote kile kilichoko katika hatua za mwanzo, waonekana uko kwenye hatua za "mpito" za kukua. Hatua ambazo kila kitu ni "mumo kwa mumo". Kama uvuvi wa kokoro ambao samaki, mawe na hata kobe wote wanakumbwa. Ni katika kipindi hiki ambacho twasema "viache vyote viote kisha magugu yatajitenga na mazao"
Ninalomaanisha hapa ni kuwa kuna blogs za wenye kujua kwanini wanafanya wafanyalo na pia kuna za wale wanaosaka kujua wanalopenda na kutaka kufanya na kuna za wale wafanyao wanalofanya kwa kuwa wenzao wanafanya ama kwa kuwa wana "access" ya kufanya wafanyalo.
Lakini leo hii, mmoja kati ya "wakongwe" (kwa muda ambao blogu zetu za kiswahili zimekuwa "hewani") anajivunia kuona blogu yake ikitimiza miaka 3. Kaka Fadhy Mtanga anaye-blog kupitia Blog ya MWANANCHI MIMI na ile ya DIWANI YA FADHILI amekuwa mshiriki mzuri wa kuonesha na kufikirisha dunia juu ya kile kilichopo "upande wa pili".
Na leo hii, blogu hii pendwa ya MWANANCHI MIMI inatimiza miaka mitatu. Sikuwa mfuatiliaji wa blogu wakati inaanza lakini nilikuja kutambua umuhimu wa blogu hii na tangu nijiunge nayo, nimejifunza na kujivunia meengi kuhusu kazi za Kaka Mtanga.
Ni kwa sababu hii na ile ya kuthamini michango ya watu mbalimbali nchini kulikonifanya kumuomba kaka Mtanga kutumia jina lake kama kipengele kimojawapo ndani ya blogu yangu ambacho hujikita katika kuonesha kile nijuacho juu ya watu ambao wamejitolea kunufaisha jamii nzima.
Ni katika kutimiza miaka hii mitatu ya blogu hii ya MWANANCHI MIMI ninapoojumuika na kaka Fadhy na wana-changamoto wengine kutafakari muelekeo wa wanablog / wananchi sisi.
Tujiulize tuliko na tupendako kwenda na hata namna tunavyoweza kukamilisha hilo.
Kaka Fadhy tuko PamoJAH na naamini kwa ushirikiano uutoao mara zote, TUTAFIKA TUUU.
Happy Third Birthdate MWANANCHI MIMI BLOG. Let's Keep On Moving

5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hongera kaka Fadhy!

Fadhy Mtanga said...

Kuna nyakati katika maisha yangu hujikuta naishiwa maneno. Hususani pale ninapotendewa jambo kubwa sana kama hili. Kaka Mubelwa, naomba upokee shukrani zangu za dhati kabisa. Mungu akubariki sana wewe na familia yako.

Da Mija nakushukuru sana kwa moyo wangu wote.

Ahsanteni sana wadau kwa kunisaidia kufika hapa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

HONGERA SHAABAN R>

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana mtani!

Fadhy Mtanga said...

Nimepita tena kuwashukuru nyote mlionitakia kila la kheri.

@kaka Kamala nashukuru sana. Ila hilo jina ni kubwa sana kwangu. Sijafikia saizi yake. Lakini nitajitahidi kujibidiisha katika ushairi wa Kiswahili ili nami niweze kuacha urithi kwa vizazi vijavyo.

@dada Yasinta, ubarikiwe sana dada wewe!

Mkuu Mutiba, pamoja daima kaka.