Thursday, April 1, 2010

Tangazo la msiba..TORONTO, CANADA

Marehemu Dada Evelyn Gembe
Familia ya Bwana na Bibi Gembe wa Upanga-Dar-es-salaam na Tabora, wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Evaline Gembe (pichani) kilichotokea hapo juzi tarehe 30.3.2010 huko Toronto,Canada.Evelyne amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa dada yake, Julie huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka. Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika.
Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : CIBC (Canadian Imperial Bank of Commerce)

ACCOUNT NUMBER: 5681839
TRANSIT NUMBER: 00902
INSTITUTE NUMBER: 010
SWIFT CODE: CIBCCATT

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwa Sania Esmail.Anuani yake ni saniae@yahoo.ca au kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:
1025 SCARLETT ROAD, APT 606, BUZZ # 178
TORONTO ON, M9P 3V3.Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Julie +1 416-247-8318
Esmail Manambi- +1 647- 299-2572
Victor Wambura- +1 647-428-4118
Prosper Luteganya- +1 905 626 3764


Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Amen.

No comments: