Thursday, May 27, 2010

Ubaya wa uzuri ni UZURI WAKE.

*Umeshajiuliza kinachowafanya watoto wa WACHA MUNGU kutoshitukiwa pale wanapomkacha Mungu? Ni kwa kuwa wazazi wamewalea katika misingi ya kutodanganya na KUAMINIWA na hivyo wanatumia UZURI wa kuaminiwa kutenda MABAYA kwa kuaga wanaenda kwenye shughuli isiyo sahihi.
*Umeshawaza hatari kubwa inayozikabili nchi zenye amani? Ni kuwa kwa kuwa na amani hiyo, nchi hizo haziwezi kuwekeza pesa nyingi kwenye kujihami na vita na matokeo yake ni kuwa wanaposhitukizwa, inakuwa ni maangamizi. Yaani UBAYA wa amani (ambayo ndio UZURI) ni amani yenyewe.
*Ati sehemu ambayo haijawahi kuwa na matukio ya wizi ndio yasemekana kuwa rahisi kuibiwa kwa kuwa waishio huko hawana mbinu nyingi za kukabiliana na wizi huo na hata kuwanasa wezi hao. Kwa maana nyingine UZURIwa kutokuwa na wezi ndio UBAYA wa eneo hilo kwa kushindwa kujiandaa na wabaya hao.
*Ati watoto "wapole" ndio wanaoonewa mashuleni na kwenye sehemu nyingine kwa kuwa tu ni wapole. Upole / kutopenda ugomvi ambako ni kUZURI kwasababisha watoto hao kuonewa ambalo ndio UBAYA wa UZURI walionao
*Naona wananchi wasiopaza sauti zao kuhusu mali wanyonywazo na viongozi, wanazidi kunywonywa kwa kuwa tu (ni wazuri) hawasemi
YAANI NAONA NAMNA AMBAVYO UBAYA WA UZURI NI UZURI WAKE

5 comments:

Koero Mkundi said...

NAKUNUKUU KAKA:

"Naona wananchi wasiopaza sauti zao kuhusu mali wanyonywazo na viongozi, wanazidi kunywonywa kwa kuwa tu (ni wazuri) hawasemi"

Hilo linawezekana kaka, lakini kumbuka wafilipin waliteswa sana na Fernand Marcos na kwa ushirikianao wa mwanamama Quarazon Aquino walimudu kuandamana hadi ikulu ambapo peoples power ilifanya kazi ya kumuondoa ibilisi yule....

Lenye mwanzo halikosi kuw ana mwisho kaka, na mwisho wa ubaya ni aibu...bado kitambo kidogo watafedhekeka hao.....

Simon Kitururu said...

``Ubaya wa uzuri ni UZURI WAKE´´

-hapo umemaliza Mkuu!

Maisara Wastara said...

Lipo jambo nimejifunza hapo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi sana, na ninafikiri wewe mzee wa c/moto ni mkristo na kumbuka Kristo alitufundisha kuwa wapole kama Ua, na akasema akupigaye kushoto mgeuzie kulia nk

kumbuka kristo alikuwa maarufa kwa kuwa alikubali kufanyiwa ubaya wa kila aina kwa hiyo ubaya waweza kuwa muhimu kuliko ukweli

hata nyerere anasifiwa kwa kuwa tu aliwafukuza wabaya nknk


ubaya juuuuuuuuuuuu

Unknown said...

Hata hiyo amani inayotufanya tuwe watu wa amani hata pale tunaponyonywa wazi wazi. Alianza mkoloni na sasa sisi kwa sisi na amani imetufanya tuwe watulivu!! Ati?? Ooh okay mazezeta!!!(ashkum)