Wednesday, July 7, 2010

NI SISI WENYE SULUHISHO LA AFRICA

Mara nyingi tumekuwa tukisaka suluhisho la matatizo ya bara letu ilhali tunasahau wajibu wetu katika kusaka suluhisho hilo. Hapa aktika video hii hapa chini, mwanadada huyu Ory Okolloh anayeendesha blog ya Mzalendo anaeleza namna Afrika tuonwavyo na wengine na uhalali wa kuonwa ama kuonekana hivyo na hata namna tunavyonyanyasana na mwisho ni ni nani wa kusukuma mabadiliko tuyatakayo.
Shukrani kwa Da Mija "aliyenionjesha" hii nilipokuwa adimikoni na sasa naamini ni wakati muafaka wa kushirikiana nanyi video hii.
TAZAMA, SIKILIZA, JIFUNZEJICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

japo siwezi kuiona hiyo video lakini jambo hili hata mimi nimekuwa nikilisema mara kwa mara. sio viongozi wetu bali sisi yaani mimi na wewe

Mija Shija Sayi said...

Inabidi tuzidi kupiga kelele bila kuchoka hadi kila Mwafrika ajue kwamba yeye mwenyewe ndiyo suluhisho.

Namsubiri kakaangu Nyahbingi hapa.

Yasinta Ngonyani said...

umefika wakati wa sisi sasa kuamka kutoka usingizini na kuanza kuijenga nchi kuanzia mawazo.Nina imani tukishikamana basi tutafanikisha tu. Pamoja Daima

EDNA said...

Africa bila umasikini,magonjwa,njaa,vita inawezekana....mabadiliko ya Africa yako mikononi mwetu tunapaswa kuamka na kuanza Kuijenga Africa yetu iliyobomoka.
Tukiondokana na chuki,ubinafsi na uroho wa madaraka hakika naamini tutaijenga Africa.