Sunday, October 17, 2010

Mwalimu Nyerere aenziwa Marekani

Jumamosi ya Oktoba 16, waTanzania, waAfrika na waMarekani wenye asili ya Afrika walijumuika katika kukumbuka kazi na Maisha ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Katika sherehe hizo, zilielezwa kazi za Mwalimu Nyerere, umuhimu wake kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Maajar, alieleza kazi kuu alizofanya Mwl Nyerere ikiwa ni pamoja na kuunganisha umoja kwa nchi yenye makabila 120, dini mbalimbali, na kuhimiza lugha ya Kiswahili na pia kusaidia kuunganisha Afrika kama anavyosema hapa chini

Baada ya maonesho nilibahatika kuongea na Balozi Mwanaidi Maajar kuhusu ufahamu wake juu ya Mwalimu Njerere na pia ambacho anaamini Mwl angekemea kama angekuwa hai

Lakini pia tulipata nafasi ya kusikiliza WOSIA kutoka kwa Brother Hodari Abdul Ali, mMarekani mwenye asili ya Afrika aliyezungumzia ziara yake ya Tanzania akiwa mwanafunzi, uelewa wake kuhusu Tanzania, Afrika na pia umuhimu na faida ya ushirikiano kati ya waTanzania na waMarekani wenye asili ya Afrika.
Bwn Hodari ni Mkurugenzi wa Give Peace a Chance Coalition (G-PAC), mtangazaji wa WPFW Pacifica Radio na mmiliki wa duka la vitabu liitwalo Dar Es Salaam lililopo Maryland nchini Marekani.

Na hizi hapa chini na baadhi ya kumbukumbu zilizonaswa na kamera ya blogu hii
Waandaaji na wafanikishi wa kumbukumbu ya maisha na kazi za mwalimu wakiwa na Balozi Maajar
Bwn na Bibi Tingling
Bwn Hodari. Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyebahatika kwenda Tanzania na kuonana na Mwl Nyerere miaka ya 70. Na sasa ana suka la vitabu liitwalo Dar Es Salaa. Alikuwa akitoa neno
Mkuu wa Ukimwi Orphans Dr Lutayuga akitoa hotuba
Balozi Maajar na Afisa wa ubalozi Suleiman Saleh wakifurahia maonesho ya mavazi ya wabunifu saba wa nchini Tanzania waliowakilishwa na Khadija Mwanamboka kama yaonekanavyo hapa chini

Waonesha mitindo / mavazi wakiwa katika picha ya pamoja

Baada ya maadhimisho nilipata nafasi ya kuhojiana na Khadija Mwanamboka kuhusu kazi ya ubunifu. Alipoanzia, alipo na anapoelekea.
Huyu hapa chini Khadija Mwanamboka

1 comment:

Subi Nukta said...

Asante KUBWA saaaaana Mubelwa. Yaani ile THANK YOU BIIIIG kabisa.