Sunday, March 27, 2011

ASIFIWE NGONYANI (1989- 2011). Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu

"..see you in ZION, holding hands together standing by MY FATHER'S SIDE. Meet you in ZION singing songs together....." LUCIANO Ni mwaka mmoja na siku 24 tangu ilipobandikwa MAKALA HII YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUFANIKISHA UPAUSAJI WA Dada Mdogo Asifiwe Ngonyani. Leo hii NAMSHUKURU MUNGU kwa maisha na mapumziko ya Dada Asifiwe, ambaye aliaga dunia Machi 23 na kuzikwa Machi 26.
Dada wa Asifiwe, ni Da Yasinta Ngonyani. Sio bloga mwenzangu tu, bali ndiye anayewasiliana na familia yangu kuliko bloga yeyote. Twawasiliana kwenye chat, kwenye simu na hata skype ambapo huwa tunaongea mara kwa mara.
Mara nyingi tumezungumza kuhusu Asifiwe. Na kila mara alikuwa akitujulisha maendeleo yake. Na kwa kila wakati ambao afya ya Da Asifiwe ilikuwa ikihitaji msaada wa uangalizi wa watabibu, Da Yasinta alikuwa mnyonge. Na nakumbuka siku ambayo alisema hakuweza kuweka bandiko kwenye blogu yake kwa kuwa hakuwa na furaha. Baadae tukawasiliana kuwa ameweza kuongea na Asifiwe na alikuwa na furaha kusika maendeleo yake ni mema.
Lakini juma hili, taarifa zimefika kuwa ASIFIWE HATUNAYE. Binafsi niliumia sana. Nilikuwa sijapata kuonana na Asifiwe, lakini mazungumzo juu yake kutoka kwa Dadake na Da Koero yalinifanya kuwa karibu naye kwa namna ya pekee.
Lakini kwa wote hawa (Yasinta na Koero), nililogundua ni namna ambavyo FURAHA ZAO ZILIATHIRIWA NA HALI YA ASIFIWE. Kwa maongezi nao, niligundua juu ya maisha yake ambayo ndicho kilikuwa kivutio kikubwa kwa ndugu zangu hawa ambacho ni TABIA. Da Yasinta hakuwa tu akimzungumzia Asifiwe kama ndugu yake ambaye ni wao wawili pekee wa kike katika familia, lakini alikuwa akimzungumzia kama RAFIKI.
NA HILI NDILO NILILOJIFUNZA NA NINALOJIFUNA.
Ninapomuwaza ASIFIWE, nikimuwaza Dada Yasinta na dugu, jamaa na marafiki wakimlilia, naona AKISI YA MAISHA YA ASIFIWE. Naona jambo ambalo sisi sote twatakiwa kujifunza kutoka kwa Asifiwe, kisha kuona maisha yetu na ya wali walio kwetu yakibadilika.
KILIO cha kumlilia Asifiwe ni ishara nyingine kuwa alipendwa, na licha ya kuwa ni KAZI YA MUNGU kumpumzisha baada ya kuyagusa maisha yetu kwa namna alivyoyagusa, bado tungependa kuendelea kuwa naye.
Nakumbuka Juni mosi mwaka 2009, NILIBANDIKA MAKALA HAYA KUHUSU KILIO CHANGU KWA MJOMBA WANGU, ambaye nililia kwa kuwa nilimlilia, na katika makala hiyo, niliandika kuhusu kilio cangu kwa mjomba kuwa "nililia kwa kuwa kwa tafsiri yangu, kulia ni kutokubali kuwa wakati wa mjomba kupumzika ulikuwa umefika na hakika alistahili kupumzika baada ya kutenda mema mengi tena kwa mapambano ya hali ya juu. Mjomba alikuwa mtu mwema kwangu na kwa wengi..." Mtu wa kwanza kutoa maoni kwenye bandiko hilo (kama ilivyo kwa mabandiko mengi kwenye blogu nyingi) ni Dada yangu Yasinta ambaye alisema "Mzee wa Changamoto pole sana tena sana. Nalia pamoja nawe kwani nakuelewa kabisa. Na nakushauri lia sana kwani kulia ni moja ya kutoa uchungu wako. Natumanini Mjomba wako yupo nawe kila siku amini. Astarehe kwa amani."
Leo hii nami namkumbuka Asifiwe, na licha ya kuwa NAMLILIA, bado nakumbuka kuwa ALISTAHILI KUPUMZIKA na kuwa aligusa maisha ya waliohusiana na kuishi naye na yetu tuliomfahamu kupitia ndugu na marafiki.
Lililo kubwa kwetu tuliobaki, ni kuishi maisha sahihi na maisha yaliyo mema. Kama ambavyo aliishi ASIFIWE NGONYANI....Na ndio maana (kama kisemavyo kichwa cha post) namuona "ASIFIWE NGONYANI kama Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu"
Chris Rice anasema....COME THOU FOUNT

NA BERES HAMMOND anasema I'LL LIVE AGAIN

6 comments:

Fadhy Mtanga said...

najikuta naishiwa maneno. Najikuta naishiwa nguvu. Lakini sisi binadamu ni nani hasa hata tukamwamulia Mungu? Kazi yake Mola daima haina makosa.
Apumzikw kwa amani mdogo wetu Asifiwe Ngonyani.
Amina.

Unknown said...

USIJALI DADA YASINYA NA WOTE WALIOKUTWA NA HALI KAMA HII.

YOTE HAYO YALISHAPANGWA, HIVYO HAYANA BUDI KUTOKEA KAMA TUJUAVYO HISTORIA YA MWANADAMU NA KISA CHA SHIDA ZOTE HIZI, ILA IPO SIKU YATAKOMA.

HATA HIVYO NIMEFANYA MUENDELEZO WA FARAJA KWA KUZUNGUMZIA JAMBO HILI KWA NAMNA INAYOTIA MOYO KWA JINSI NILIVYOGUSWA.

http://mtayarishaji.blogspot.com/2011/03/je-unajua-yanayotokea.html

TUPO PAMOJA WOTE.

Rachel Siwa said...

@kaka Mubelwa[babap]maneno yako ni mazito sana na yenye kuvutia na upendo mwingi!Ubarikiwe sana na Poleni sana,Mungu anamakusudi ya kukutanisha watu wake iwe kwa kuonana au kwa mawasiliano.

Simon Kitururu said...

R.I.P Asifiwe!

Yasinta Ngonyani said...

Nona yote yamesemwa nami nachotakiwa kusema ni AHSANTE SANA. Mwenyezi Mungu ana awazidishie upendo mara mia. <<<<<<<PAMOJA DAIMA!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Apumzike salama huyu binti.