Sunday, May 8, 2011

Kwa Mama yangu, Mamaa wangu, Mama wa kwetu na Mama zetu

ASANTENI......Katika MAISHA YANGU, kila mtu ana umuhimu. Na kila mtu ni sehemu ya ukuaji wangu japo umuhimu na ukuaji huo waweza kuwa ama kuja kwa aina na malengo tofauti. Lakini "mwisho wa siku" nakuwa nimejifunza na nimeerevuka zaidi ya nilivyokuwa kabla. NDIVYO NIFAHAMUVYO KUHUSU MAISHA.
Lakini pia nataka kukiri kuwa maisha yangu ya kila siku yamekuwa zao na endelezo la kinamama ambao katika ngazi na matukio mbalimbali maishani wamekuwa sehemu kubwa ya suluhisho. Simaanishi kuwa kinababa hawapo (kwani kinamama hawa wamekuwa walivyo kutokana na kinababa walio upande wao), lakini kwa kuwa leo ni siku ya kinamama hapa Marekani (naamini haiadhimishwi pamoja duniani kote), naomba nizungumzie nafasi yao maishani mwangu. Mama yetu.....HAKUNA KAMA YEYE. Mama wa kwetu (dada zetu) ambao wote sasa ni WAZAZI. Nawapenda nyooote na nawatakia kila siku iliyo ya mafanikio kwani kwangu mimi, kila siku ni siku yenu, ni siku niwakumbukao na kuwaombea.
Kwanza nianze na Mama yetu mpeeenzi. Ambaye katika miaka 18 ya mwanzo maishani mwangu amekuwa MSINGI IMARA wa mimi kuwa nilivyo. Beres Hammond alipata kuwaelezea wanawake akisema kwa wakati mmoja, mwanamke anaweza kuwa "tough as a rock, but soft like a rose petal". Na hayo nayaona kwa Mama yetu. Kwa nyakati tofauti nilidhani kuwa sahihi zaidi yake lakini baadae nilikuja kuelewa kwanini amekuwa namna alivyo na kwanini alitenda alivyotenda na mwisho kuwaza "kwanini alitenda yoote aliyotenda kwa ajili yangu? SINA NINALOWEZA KUMUOMBA MUNGU ANIONGEZEE KWA MAMA YANGU.
Lakini pia kuna Mama mkwe wangu (ambaye leo nayarejea malezi yake kwa kutumia mwanae ambaye ni mke wangu na ambaye anaakisi maisha halisi aliyokulia). Mama huyu ndiye aliyeleta kile niitacho FURAHA YA KWELI maishani mwangu. Amelea mtu ambaye sasa ni suluhisho halisi na kila nimuangaliapo mke wangu na kuzungumza na Mama Mkwe wangu nahisi mwenye BARAKA ya kipekee kupokea "tunda la malezi yake". Mamaa wangu. Mama wa mwanangu na "stress buster" wangu. Ndio....MKE WANGU..... HAPPY MOTHER'S DAY
Nirejee kwa Mama wa mtoto wangu. Huyu ndiye "STRESS BUSTER" kwangu. Ni makao makuu ya furaha yangu na dampo la mawazo yangu. Kwa huyu sina ninaloweza kusema mengi kwani ndiye anifanyaye niendelee kuwa vile ambavyo wazazi na walezi wangu waliweka msingi huo.
Maisha yangu yalipitia malezi ya Mama zangu wadogo na Dada zangu. Hawa nao ni sehemu kubwa ya maisha niliyo sasa. Nikiwa mhangaikaji asiyeonekana kuwa na mafanikio ya karibu maishani, waliendelea kunishauri, kunipa moyo na kunisaidia katika kile nilichoamini kuwa ni fanikio langu lijalo. Kwa asilimia kubwa najivunia uwepo wao na kwa kuwa kwa pamoja wote wamekuwa MSAADA MNYOOFU kwangu kwa kuwa na suluhisho lisilohitaji mimi kudhihirisha kitu ili kulifikia. WALIKUWA, WAMEKUWA NA NAAMINI WATAENDELEA KUWA UPANDE WANGU.
Lakini pia nina Dada wadogo ambao nao kwa nafasi waliyokuwa nayo walikuwa chachu saana ya mimi kufanikisha nitakalo. Nakumbuka nikiwa Times Fm kuna wakati ambao "feedback" pekee ambayo ningeipata ni kutoka kwa Kaka na Dada zangu wadogo ambao walijitahidi kunisikiliza kila uchao na kunipongeza ama kunicheka "nilipochemsha" jambo ambalo liliongeza ufanisi kwangu. Kwa hiyo kwa kina Dada Abeella, Byela, Atu, Juliana na wengine (ambao mmeshakuwa Mama Wadogo na mashangazi), nawashukuru, nawapenda na natambua kuwa mmekuwa sehemu kuu ya changamoto zilizonifikisha hapa nilipo.
Kuna Dada zangu wa hiari ambao kiiiila siku nawasiliana nao. Iwe ni kwa kusoma kwenye mitandao yao ama wao kusoma kwangu. Iwe ni kwa kuwasiliana kwenye facebook, messenger, msn ama aina yoyote ya mawasiliani ya kijamii. NAWAPENDA SAANA.
Mmekuwa nguzo muhimu ya kile nionacho kama mafanikio na mmefanikisha kuboreka kwa HIMAYA HII ambayo ni sehemu ya maisha yangu pia. Kwa kina mtabibu wa blog, Dada Subi, Da Yasinta wa Maisha na Mafanikio na Dada "muamshaji" Koero wa Vukani, Da Sophy wa Bambataa, Dada Agnes wa Kiduchu, Da Sarp wa Angalia Bongo, Da Faith wa "Ulimwengu Mdogo", mwanamke wa shoka Da MiJAH, Dadangu Dina wa Marios, Da Edna wa "mchakato wa maisha" (strive for life), Dada Happy Katabazi uwapaye hofu viongozi kwa kalamuyo, Dada Jackline Charles, Dada mpiganaji Judith Wambura, Dada zangu wajasiriamali Marium Yazawa na Shamim wa Zeze, Dada mwenye wito wa mitindo na mavazi Scola wa Passion4fashion, mshairi wa kutazama Upande wa Pili Da Serina, Dada Sophie wa Sophie Club, Dadangu Mpenzi Mary Damian na Da mkubwa Chemi wa Swahili Time. Dada-Rafiki Makrina a.k.a Mama Paul nawe shukrani kwa uwepo wako.
Kwa kinamama nyooote mliogusa maisha yangu kwa namna yoyote ile, nawapenda na kila siku naona na kudhihirishiwa thamani yenu. Lakini leo kwa kuwa wametenga siku ya kuwaenzi hapa, NAWAOMBEA MAFANIKIO KATIKA KILA JEMA MTENDALO.
Kwa kinamama mlioonesha njia sahihi tangu awali, twawashukuru kwa mwanga mliotuwashia.
Kwa kinamama ambao mnatufunza kuhusu "upande wa pili wa dunia" nanyi pia twashukuru kuwa uwepo wenu watukumbusha kuwa dunia haijajazwa na wale watendao tupendayo tu. Mwanamke wa shoka (mtarajiwa) Paulina. AKISI ya kinamama wengi waliotulea sisi wazazi wake
Kwa kinamama watarajiwa, twatambua mwajifunza njia sahihi na twaamini mtaonesha usahihi huo wakati ukifika.
Lakini kwa ujumla wake, HAKUNA KAMA MAMA.
Msikilize Beres Hammond anaposema "What a woman"

7 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongereni akina mama. Tunawaenzi !!!

Simon Kitururu said...

Hongera zenu akina MAMA sana tu!

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana akina MAMA. Pia nachukua nafasi hii kwa kupata heshima katika kibaraza hiki cha Changamoto . Ahsante na akina mama wote wuwe na siku nzuri leo.

Rachel Siwa said...

Hongera mama P,na kina wote pamoja na mimi mama S!.

Mwanasosholojia said...

Umenena yote mkuu, hongera kwa akina mama!Wao ni kila kitu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bamawe mwaihukage kasinge kutuzala nakutua ebunura

emu-three said...

Nilikuwa wapi sikusema lolote hapa...mmh, TUPO MKUU NDUGU YANGU!