Tuesday, July 12, 2011

Tanzania Yangu.....Iliyo "bize" kumwagilia matawi badala ya mizizi (II)

Novemba 27, 2009 niliandika sehemu ya kwanza ya bandio lenye kichwa kama hiki. Japo si katika maudhui yanayofanana kabisa, lakini naamini bado kichwa hiki kinafaa hapa. Na pia nikumbushe kwamba Februari 2, 2010 niliandika kuhusu WAKUU WA MIKOA nikiuliza kama ni watumishi wa wananchi ama ni mzigo kwa serikali na wananchi? Pia nikaeleza niaminivyo kuwa ni CHANZO CHA KUDIDIMIA MAENDELEO MIKOANI
Na leo ningependa kuiangalia mikoa yenyewe.
Maendeleo yake na namna yapatikanavyo. Na mengine mengi
Nimekuwa nikiwaza kuwa MIKOA ina mahitaji mbalimbali na inahitaji pesa kuyatimiza.
Ni vipi inapata pesa zake? Na wapi inapopata?
Katika "bandiko" langu kuhusu WAKUU WA MIKOA, nilisema "NALOAMINI NI KUWA, Endapo wakuu wa mikoa wangekuwa wanagombea basi wangekuwa na ubunifu wa kutumia rasilimali zilizopo mikoani ili kukamilisha bajeti na mahitaji ya mikoa wanayoiongoza na kupunguza kutegemea ruzuku za serikali kuu. Mikoa yetu ina rasilimali nyiiingi na kama ingetakiwa kujiendesha kwa kujitegemea nina imani kungekuwa na ubunifu na uchungu wa kutumia rasilimali hizo. Lakini kwa sasa sioni kazi za wakuu wa mikoa kwa sababu ndani ya miaka mitano ya Rais, wengine wanakuwa wameshahama "vituo" vya kazi zaidi ya mara mbili na hakuna la maana wanalofanya kuiendeleza. Naamini ni mzigo kwa serikali na wananchi kwa ujumla."
Bado naamini hivi. Sijawahi kusikia BAJETI YA MKOA fulani na kama ipo sina hakika kama hutofautishwa kulingana na mahitaji. Yawezekana Dar Es Salaam ikawa na bajeti kubwa ya ulinzi (kutokana na wageni wanaoitembelea) kuliko Rukwa, lakini ni nani ajuaye? Ni kipi chanzo cha mapato cha mikoa hii na ni nani anayepanga bajeti yake? Ni yupi anayetoa uwiano wa kiasi gani kiende wapi ikiwa fedha za KUENDESHA MIKOA zinatoka serikali kuu? Na kama ndivyo, ni kweli kuwa Mbeya (waliomrushia Rais mawe) watapata fursa sawa ya kipato sawa na Pwani? Na je, mikoa kama Arusha ambao wana rasilimali nyingi ambazo wangeweza kuzitumia kupata kipato cha mkoa na kuendeleza shughuli zao, watapata fungu sawa licha ya kuwa na wapinzani wengi bungeni?
Ni kweli kuwa mikoa kama Arusha ama Shinyanga na hata Mara inastahili kuwa na shida kwenye shule zao kama mikoa mingine? Naamini kama wangekuwa na bajeti zao, na kutenga fungu kutokana na makusanyo yao, na kugawa makusanyo kulingana na mahitaji yao, basi shule katika baadhi ya mikoa zingekuwa bora, barabara zisingefanana na mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za mikoa isingechelewa.
Ni kweli kuwa tunaweza kujenga serikali kuu bila kujenga ngazi za chini?
Ni kweli tutaweza kudhibiti na kuwa wazi katika bajeti ya serikali kuu kama hatujui ya mkoa?
Wananchi wana nguvu ama maamuzi gani kuhusu bajeti ya mikoa yao?
Matumizi yake je? WANASHIRIKISHWA?
Katika Hotuba ya Mwaka Mpya 2011 ya Rais Jakaya M. Kikwete, aligusia kile alichokiita NIDHAMU YA MATUMIZI ambapo alisema (na hapa namnukuu) "Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa nidhamu ya matumizi bado hatujapiga hatua ya kunifanya nipoe moyo, ingawaje kuna mafanikio yanayoendelea kupatikana. Niliwakumbusha Mawaziri kuhusu kuwepo Kamati za Matumizi ya Fedha katika kila Wizara, Idara za Serikali na Halmashauri za Wilaya na Miji ambazo niliagiza ziundwe miaka mitatu iliyopita.

Niliwakumbusha kuwa, wakuu wa taasisi hizo ndio wanaoongoza Kamati hizo na hivyo wao ndiyo wanaoongoza Kamati za Wizara zao. Nimewataka wahakikishe kuwa Kamati hizo zinatekeleza ipasavyo majukumu yake ili rasilimali za taifa zifanye kazi iliyokusudiwa. Halikadhalika, niliwataka wahakikishe kuwa Kamati za Idara na Mashirika chini ya Wizara zao zinafanya kazi kwa ukamilifu.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji, mwaka huu tuliendelea kuziimarisha Idara za Uhasibu na Ukaguzi wa Ndani. Tutaendelea kuhakikisha kuwa kila Halmashauri ina Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wenye ujuzi na sifa zinazostahili za kitaaluma, uaminifu na uadilifu."

Kama tunataka kujenga serikali kuu iliyo na NIDHAMU YA MATUMIZI, ni lazima kuwa na NIDHAMU YA MATUMIZI katika ngazi zote za utawala.
Lazima tujue kuwa wengi wa wafanyakazi / watawala walio serikali kuu wametoka ngazi za chini. Na bila kuwaengea UAMINIFU NA UADILIFU katika hatua za awali, tusitegemee kuwa na serikali kuu yenye UADILIFU.
Ni wakati wa kujua kuwa licha ya kwamba matokeo ya utendaji m'bovu yanaonekana kama maamuzi ya serikali kuu, lazima tujue kuwa kurekebisha hilo kwahitaji ngfazi za chinbi. Kama ambavyo tunaona majani yakikauka tukamwagilia mizizi.
TUONANE "Next Ijayo"

3 comments:

Simon Kitururu said...

Natamani kweli mpaka Pinda na Kikwete wangekusoma katika hili!:-(

Albert Kissima said...

Kaka, uchambuzi wako ninaukubali. Kwa utaratibu mbovu wa serikali yetu, haishangazi kuona palipo na mabwawa ya maji kwa ajili ya kufulia umeme au palipo na makaa ya mawe au gesi hakuna nishati ya umeme ama ni ya kusuasua.
Haishangazi pia kwa vijiji fulani kuishia kuona tu nyaya za umeme zikiambaaambaa tu hewani kuelekea kwa wakubwa fulani au kwenye kiwanda fulani. Kulingana na tathmini yangu, kipindi fulani cha nyuma barabara zilijengwa kwa kutegemea eneo fulani kuna nini cha muhimu. Kama hakuna hospitali kubwa, au kiwanda au mgodi, au ni barabara wapitayo watalii kuelekea hifadhini n.k basi wananchi walio maeneo yasiyo na maslahi kupata barabara zenye ubora inakuwa ni ndoto. Lakini ndio Tanzania yetu. wa serikali yetu, haishangazi kuona palipo na mabwawa ya maji kwa ajili ya kufulia umeme au palipo na makaa ya mawe au gesi hakuna nishati ya umeme ama ni ya kusuasua.
Haishangazi pia kwa vijiji fulani kuishia kuona tu nyaya za umeme zikiambaaambaa tu hewani kuelekea kwa wakubwa fulani au kwenye kiwanda fulani. Kulingana na tathmini yangu, kipindi fulani cha nyuma barabara zilijengwa kwa kutegemea eneo fulani kuna nini cha muhimu. Kama hakuna hospitali kubwa, au kiwanda au mgodi, au ni barabara wapitayo watalii kuelekea hifadhini n.k basi wananchi walio maeneo yasiyo na maslahi kupata barabara zenye ubora inakuwa ni ndoto. Lakini ndio Tanzania yetu.