Friday, November 25, 2011

A NEW DAY.......Luciano

Photo Credits: greetingcarduniverse.com
Maisha yetu yameandamwa ama yameambatanishwa na matukio ya aina mbalimbali. Na kila uchao, matukio hayo hutufanya tuwe tunavyokuwa. Kama ambavyo nimekuwa nikiamini kuwa "WE'RE WHO WE ARE BECAUSE OF OUR PAST AND FOR OUR FUTURE". Huu ni "ukweli mtupu" ambao hakuna anayeweza kubishana nao. Kwamba umekuwa uliyekuwa ama hujawa uliyetaka kuwa kwa sababu ya maisha yako yaliyopita, na upo ulipo kutambua mustakabali wako.
Lakini haya yote yanatokea ilhali tunatambua kuwa tumezingirwa na watu mbalimbali. Watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanakuwa na tafsiri ya maisha yetu. Nakumbuka Profesa Joseph Mbele aliwahi kujibu shukrani za msomaji mmoja juu ya ELIMU YAKE KWA WASOMAJI wake naye akasema ni walimu wa shule za awali wanaofyeka misitu na wao ndio wa kushukuriwa kuliko waalimu kama yeye wanaofunza katika kiwango cha chuo kikuu ambapo wengi wa wanafunzi / wanachuo wanakuwa wameshajitambua. Hili lilinifanya nimuwaze mwalimu wangu wa shule ya awali, ambaye ndiye haswaaa aliyenitoa kwenye UTUPU wa uwezo wa shule mpaka sasa ninapoandika usomacho wewe. Na huwa nawakumbuka waalimu wangu kila nipigapo hatua ya shule. Na mwisho wa wiki hii najua ni wakati ambao ndugu, jamaa na marafiki wengi wanakabidhiwa "magamba" yao baada ya kumaliza elimu. Wanakwenda kupambana na uhalisia wa maisha (ambao mara nyingi hauakisiwi darasani KAMA NILIVYOELEZA HAPA. Na kati ya wahitimu wa mwaka huu, na ambao watakabidhiwa vyeti vyao ni wadogo zangu Amwesiga na Alindwa Bandio. Mapacha wanifuatao ambao ninafarijika kila nisikiapo juhudi zao katika maisha na shule. Amwesiga akipokea pale UDOM na Alindwa yeye akichukua chake SAUT.
HONGERENI SANA
Amwesiga, Mama wa Changamoto na Alindwa Bandio(s)
Pia Kaka-rafiki Chris Charles anapokea chetiche pale SAUT. Na alikuwa mkarimu saana kunialika na kama ilivyo kwa wengine, nasikitika saana kuwa sitaweza kushiriki. HONGERA SAANA KAKA
Chris Charles
Pia Dada-rafiki Radhia naye anaungana na wengine wengi wanaokabidhiwa vyeti. Radhia yeye ni kwenye masuala ya fedha pale IFM.
HONGERA SANA RYAH
Radhia Mbeyu
Lakini natambua kuwa ni wengi wamalizao ama wapokeao vyeti kwa kuwa wameaminiwa kumaliza vema masomo yao. Kwenu nyote muingiao katika ulimwengu wa maendeleo ya nchi, NAWATAKIA KILA LILILO JEMA. Nawaomba msiwasahau waliowafikisha hapo na pia nia hasa ya kufika hapo (ambayo naamini ni njema).
Natoa SIFA NA SHUKRANI kwa ndugu, jamaa na marafiki wote mkamilishao taratibu za KUMALIZA MASOMO YENU.
Najivunia kuwafahamu, kwani kwa utengano na umoja wenu mmekuwa sehemu ya mimi kuwa nilivyo na nawaombea mafanikio katika kila lililo jema.
Na kwa kuwa leo ni Ijumaa, ambapo burudani yetu huwa ni ya Reggae, na nimkaribishe Luciano katika kibao chake A NEW DAY ambapo anamshukuru Mungu kwa kumfikisha katika SIKU MPYA. Na amezungumzia namna ambavyo Mungu pekee anaweza kutufikisha mbali zaidi iwapo tutaendelea kumtumikia. Ni reggae ya kusikiliza zaidi, na naamini mtasikiliza huku mkiiwaza siku hii mpya. Siku ambayo inaongeza UPYA katika sehemu ya maisha yenu na pengine kufungua milango mipya ya maisha yenu.
BETTER DAYS ARE COMING.
God Bless y'all

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.

IJUMAA NJEMA

1 comment:

Jigambe Team said...

This is real true coz the journey was so far it better to have thanks to all people who are together with them especially teachers and other stake holder like parents. thanks
g.francis@jigambe.com