Wednesday, December 21, 2011

Kwa ndugu zetu wa Dar Es Salaam....POLENI SANA

May the comfort of God help you during this difficult time. Labda hatuoni na kuumizwa na yanayotokea kwao kwa kuwa HATUKO NAO. 
Labda hatuhisi uchungu wa kinachotokea kwa kuwa HATUJAPOTEZA NDUGU. 
Labda hatuoni kuwa twaweza kusaidia kwa kuwa TWADHARAU NGUVU ZILIZOMO NDANI MWETU (maombi). 
Labda tunajisahaulisha kuwa ni wenzetu kwakuwa HATUWAFAHAMU. 
Labda tunaona ni namba ndogo kwa kuwa TWAWACHUKULIA KAMA TAKWIMU. 
        Lakini ndugu zangu na wasomaji wa blogu hii, tuna tunaloweza kuwasaidia ndugu hawa. HATA MAOMBI TU YANATOSHA KUWASAIDIA. 
Hali ya Dar Es Salaam ni mbaya saaana na kwa hakika kila mwenye kuweza kusaidia na afanye hivyo. Najua kila mmoja ana matatizo yake, na mimi nina ya kwangu. 
Lakini TUKIWAWEKA KATIKA SALA ZETU TUTAKUWA TUMEWASAIDIA SAAAANA. Hakuna msaada wa mbali na usio na gharama lakini wenye nguvu kama maombi TUWAOMBEE WATU WA DAR ES SALAAM To all My Brothers, Sisters, Aunts and Uncles and everyone in Dar Es Salaam....... Although no words can really help to ease the loss you bear, just know that YOU ARE VERY CLOSE IN OUR EVERY THOUGHTS AND PRAYERS Photo Credits Michuzi Blog and Single and Sane blog

2 comments:

Unknown said...

Kila jambo lina makusudi yake, Mungu ana namna nyingi ya kutufunulia tunaoongozana nao kama sio kuongozwa nao.

Inaumiza, lakini haina namna imeshatokea na labda itaendelea kutokea...Jinsimji ulivyo!...jinsi hali ilivyo..! jinsi kila kitu kinavyochukuliwa na kuendeshwa...!!!

NINAWAZA SANA HADI NAHISI KICHWA KIMEONGEZEKA UPANA.

Mungu atakuwa anamakusudi yake tuendelea kumuuliza lakini piatushirikiane na kusaidiana.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Unasikika vizuri sana mtangazaji.

Ninaloweza kusema tu ni Amen. Mapenzi ya Mungu yatimizwe na waliopoteza maisha wapumzike salama...

Najikaza kweli nisiseme ninayotaka kusema kwani kidogo nina hasira !