Thursday, May 31, 2012

Narejea.....japo "ado ado"

Najua kuwa nimekosekana hapa. Najua kuwa nimewakosa pia. Lakini napenda kuwajulisha kuwa ni mihangaiko ya kazi na shule na familia ambayvyo vimeniweka kando. Lakini nawashukuru saaana kwa kuwa nami japo kifikra., Wapo walioniandikia kunijulia na kunijulisha hali. NAWASHUKURU Namshukuru Mungu kwa uhai wako, wangu na wa wale watuzungukao. Namshukuru Mungu kwa wale wote ambao wametangulia mbele ya haki Namshuku Mungu kwa familia yangu pamoja na ndugu na jamaa na marafiki ambao mmekuwa pamoja nami. Kama nilivyosema, nimekuwa "bize" saaana na mambo mbalimbali. Shule ambayo ilibana mpaka nikahitaji "tafu" ya mwana
Pau wangu akinisaidia kuweka script sawa ndani ya studio za chuo 
Nimefanikiwa kumaliza muhula wangu wa shule kwa furaha saana
Nimebarikiwa kupata mahojiano na watu mbalimbali.
Nimeweza kuendelea na malezi ya familia na kuendeleza fani yangu hasa na wangu rafiki Abou.
Nimerejea....japo ADO ADO
Nawe rejea nami, na karibu tujuzane yaliyojiri wakati hatuko pamoja.
Yaliyotukosesha kuwa pamoja...NI CHANGAMOTO ZETU MAISHANI
Nawapenda

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

NIFURAHAAAAAAAAAAAAAAAAAA!
Kuwa unarejea ni kweli umekosekana kwelikweli na binafsi nimekumiss. Nimeipenda zaidi picha ya Pau kwa jinsi anavyokusaidia..Haya karibu karibu sana.