Wednesday, May 23, 2012

Semina ya neno la Mungu May 24, 2012

Unakaribishwa kwenye semina ya neno la Mungu itakayofanyika siku ya alhamis, Mei 24 katika eneo la chuo kikuu cha Maryland. Katika semina hiyo, pia kutakuwa na huduma ya kusifu na kuabudu kutoka kundi linaoundwa na muunganiko wa wanamuziki wa injili wa hapa Washington DC Metropolitan pamoja na kundi la J-SISTERS na Flora Mbasha.
JINSI KUFIKA KWENYE MKUTANO. 1. Kwa wanaotumia metrol rail toka popote pale, hakikisha unapanda GREEN line hadi College Park Metro Station, kisha panda METRO BUSES (Route number F6 na C8) yatakupitisha hadi ukumbini. Shukia kituo cha LIBRARY. 2. Kwa wote wanaotokea maeneo ya Greenbelt, tumia Metro bus (Route number C2 na R3) ushukie LIBRARY. Pia kwa wote wanaotokea West Hyattsville tumia Metro bus (Routes F6 na F8). 3. Watu wanaotokea Langley Park Takoma tumia bus C2 na wanaotokea White Oak panda Metro bus C8 hadi University of Maryland, kituo ni Library. Muda wa kufika kwa wote ni saa 11jioni, Mungu awabariki sana.

No comments: