Sunday, June 3, 2012

Japo ni karatasi, lakini "imebeba ulimwengu"

Ndio..
Ni KARATASI ambayo ina maneno yasiyo "mazito".
Si karatasi ninayoweza kuombea kazi na wala si karatasi ninayoweza kulipia madeni yoyote.
Hainipi heshima kama zilivyo karatasi nyingi za wengi, lakini kwangu NI IMARA.
Na kama nilivyosema kwenye kichwa cha post, KARATASI HII INABEBA ULIMWENGU.
Kwenye kiswahili kuna msemo kuwa ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU. Sina hakika kuwa msemo huu unamaanisha kuwa afunzwaye na mamaye hafunzwi na ulimwengu, na siamini kama unamtenga "babaye" msemwaji.
Nilipata kuandika aiku ya Jumatano ya Aprili 8, 2009 kuwa HUWEZI KUWASHUKURU WOTE, WAOMBEE.
Bado naamini katika hilo.
Katika karatasi hii, kuna JITIHADA ZA WENGI, kuna USHAURI WA WENGI, kuna KUKOSOA KWA WENGI, kuna MAONI YA WENGI, kuna watu wengi ambao KWA NAMNA CHANYA AMA HASI WAMEWEZA KUNIJENGA NA KUNIJENGEA IMANI YA KUTENDA HAYA.
Ni safari iliyoanzia kwenye familia, ikakua mpaka kwa ndugu, jamaa, marafiki wa karibu na wa mbali na wale ambao waliweza kusema waliloamini ni sahihi katika kazi niliyokuwa nikiifanya.
Ni wale walionipa nafasi ya kujaribu nilichoamini kuwa ninaweza japo sikuwa na namna ya kudhihirisha UWEZO huo.
LAKINI WALINIPA NAFASI.
Ni vituo vya radio ambavyo vilinipa nafasi na imani ya kutumia "mawimbi" yao kupanua uwezo wa fikra na kutengeneza mazingira ya kukosea na kukosolewa ambako kumenijenga zaidi.
Kuanzia Times FM Dar, Jambo Radio UK, East Africa Radio USA, Pride FM Mtwara, Voice of America USA na Ebony FM.
Lakini pia hii ni AKISI ya wale ambao wamekuwa nami bega kwa bega katika nia yangu ya kukamilisha ninachopenda japo hawakuona mwanga mwema katika njia nliyochagua.
Pengine nitoe shukrani za pekee kwa mke wangu mpenzi Esther na binti Paulina ambao NIMEKUWA NIKIWATELEKEZA kuweza kufanikisha ndoto hizi, na ambao wamekuwa wakikesha nami kuhakikisha uhariri unakamilika kwa wakati na wakati mwingine kunipa moyo nikatapo tamaa.
Siwezi kumtaja kila mmoja, kwa kuwa ni jambo lisilowezekana. Nimemtaja mke wangu, lakini naye kalelewa na wazazi ambao nao walilelewa na wazazi / walezi nk. Na hawa wote wame-shape nilicho nacho sasa. Ntawakumbuka kuweza kuwashukuru?
La hasha!!!!
Wapo wale walionifanya niamini kuwa siwezi kuwa nilivyo leo. Iwe ni shule ama sauti ama muonekano n.k
Wapo ambao nimeambatana nao kwenye kazi hizi na hasa Kaka-rafiki Abou Shatry ambaye tumekuwa timu moja kwa muda sasa. SHUKRANI KWAKO MKUU.

Lakini ni nani wa kubeba SIFA hii?
Ni nani wa kustahili shukrani? Well...ni nyote, nawashukuru saana.
Na KARATASI HII, INANIKUMBUSHA MENGI KUHUSU SAFARI YANGU NA WENGI WALIOGUSA SAFARI HIYO.
Wapo nchi mbalimbali, wametawanyika saana, lakini wote, popote walipo na vyovyote walivyo nawapenda na nathamini juhudi zao.
Hii karatasi inabeba juhudi zenu. Na kwa hakika yaubeba ulimwengu

UPENDO KWENU                                                         

3 comments:

nyahbingi worrior. said...

Hongera kaka.

Mzee wa Changamoto said...

Thanks Mkuu.
Baraka kwako

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA KAKA BABA PAULINA:-)