Tuesday, July 31, 2012

Ana kwa Ana na Mhe. Dr. Faustine Ndugulile

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuketi na Mbunge wa Kigamboni (CCM) Mhe. Dr. Faustine Ndugulile kuweza kuzungumza mambo mbalimbali. Katika maelezo yake kwenye sehemu hii ya kwanza, ameeleza kuhusu kongamano kuu la UKIMWI alilohudhuria hapa Washington DC, hali ya mapambano ya UKIMWI nchini Tanzania na pia harakati zake BUNGENI. Pia akagusia mgogoro wa MJI MPYA wa KIGAMBONI na mengineyo. Katika sehemu hii ya pili, amezungumzia suala la mgomo wa madaktari na athari zake kwa nchi. Je! Yeye (ambaye pia ni Daktari) anaamini kuwafutia leseni ni uamuzi sahihi?. Tumesherehekea SIKU YA MASHUJAA NCHINI. Ni kweli kuwa Tanzania TUNA MASHUJAA? TUNAWAENZI VEMA MASHUJAA (kama wapo) na NI VIPI TUNATENGENEZA MASHUJAA WAJAO? Anazungumzia vipi vipaumbele vya matumizi ya serikali kulingana na mahitaji ya mwananchi? Ni vipi/ ama kwa kiasi gani kuna ushirikiano wa wabunge (hasa vijana) toka vyama mbalimbali ili kuipeleka Tanzania mbele Imeelezwa kuwa serikali inachangia 3% ya gharama za mapambano dhidi ya UKIMWI licha ya kuutangaza kama JANGA LA TAIFA. Ni kweli tuna dhamira ya kupambana na ugonjwa huu? Na upi mwito wake kwa waTanzania wote? KARIBU

1 comment:

emuthree said...

Mkuu twashukuru sana kwa kutujuza hayo mazungumzo tupo pamoja