Saturday, July 14, 2012

TOKA WAVUTI: Yatokanayo na msiba wa Domi: Funzo kwa wanaoishi ndani na nje ya Tanzania

 
Hii ni rekodi kutoka kwenye kipindi cha "Weekend Special" cha redio WAPO FM kuhusu yaliyotokea baada ya msiba wa Domi ambapo familia ya marehemu ilirusha madai kuhusu mali na fedha na kuweka zuio kwamba mke asiruhusiwe kusafiri kutoka Tanzania kurudi Marekani waliko watoto wake. 
 Mtangazaji wa WAPO Radio, Anthony Joseph, alizungumza na kila upande unaohusika na suala hili na kisha kuzikutanisha pamoja ili kuwekana sawa kuhusu tuhuma zilizotamkwa. 
 Dada Subi wa blogu ya WAVUTI aliweza kukisikiliza kipindi hiki na kukirekodi kwa maombi maalum na kisha kuiweka HAPA Kwa mujibu wa Dada Subi, anasema "baada ya kukisikiliza, nimejifunza mengi ambayo ningependa na wengine wajifunze na kuchukua hatua madhubuti. Changamoto za maisha ya ndoa, ughaibuni, familia na tamaduni mbili zilizo mbalimbali!" 
 NINALOWEZA KUSEMA NI KUWA...SIKILIZA NA TAFAKARI
   
NB: Kutokana na mawasiliano tuliyopata toka kwa baadhi ya waliotajwa na waliohusika katika harakati za kuuguza na kumsafirisha Domi kwa mazishi, naamini ni vema kwa ndugu hawa kupata nafasi ya kueleza UPANDE WA PILI wa habari hii kama ambavyo baadhi yao wameomba. 
NALIFIKIRIA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hii sio haki hata kidogo...

Unknown said...

Poleni wote

Unknown said...

Domitian pumzika kwa amani .Tumejifunza mengi kutokana na wewe. Msiba wako umetoa fundisho kwa wengi.Rambi rambi na mali ulizoacha haziwezi kuziba pengo uliloacha kamwe hata zikigawanywa kwa usawa wa kiasi gani! Hata michango yoooote iliyochangwa huku Washington DC ikigawanywa kama inavyodaiwa na ndugu zako naamini pia na ndugu zako walichangisha- sina hakika kama Mke wako alipewa maana hawaizungumzii nayo igawanywe sawa kama wanavyotaka - Wewe hutarudi - PUMZIKA KWA AMANI DOMI!!!
JAMANI MWACHENI DOMI APUMZIKE!!!!