Thursday, August 9, 2012

Siku yangu.....AKISI YAKO


JAPO NI KUMBUKUMBU YA SIKU YANGU MUHIMU, lakini bado siku hii ni AKISI YA UWEPO WAKO.
Nilizaliwa, lakini sikuwa nilivyo sasa. Niko nilivyo kwa sababu ya mazingira yanizungukayo, na mazingira hayo yako yalivyo sababu ya jamii iliyomo. Jamii ituzungukayo ni uchaguzi wa fikra zetu, na fikra hizo ni zao la jamii hiyo.
NGUMU KUMEZA, lakini ndio ukweli...
Kuwa "Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii" NAJIVUNIA KUWA NA JAMII NILIYONAYO. NAJIVUNIA KUWA NAWE KAMA RAFIKI.
Nipo nilivyo sababu ya uwepo wako kwangu. Na ninapokumbuka siku yangu ya kuzaliwa, naakisi vile nilivyo nikiona NAFASI NA THAMANI YAKO MAISHANI MWANGU NAKUPENDA, NAKUHESHIMU NA NAKUTHAMINI SANA.
Asante kwa kuwa wewe.
Asante kwa kuwa nami.
BARAKA KWAKO

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA NA MWENYEZI MUNGU AKUZIDISHIA UPENDO NA AKUJALIE JINSI UNAVYOJALI WENGINE. BABA PAULINA NIMESIKITIKA UMEMTENGA PAULINA SIJAMWONA:-).. UWE NA SIKU NJEMA SANA.