Saturday, August 25, 2012

Uzinduzi wa tawi la CCM DMV leo

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tawi la CCM hapa DMV Mhe. Abdulrahman Kinana amewasili jana na kulakiwa na na viongozi wa matawi ya CCM DMV na New York.
Kushoto ni Katibu wa Tawi la CCM DMV Bw. Jacob Kinyemi, Katibu wa Tawi la New York Bwn. Shabani Mseba na Mwenyekiti wa Tawi CCM DMV Bi Loveness Mamuya.

Mhe Abdulrahman Kinana, ambaye ni kanali mstafu wa jeshi, ni mmoja wa wanasiasa wakongwe na mahiri nchini Tanzania. Ni mjumbe wa taifa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki na Meneja wa Kampeni wa Mhe Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.
 Ufunguzi wa Tawi la CCM unafanyika leo Jumamosi Aug 25, 2012 katika ukumbi wa Martin Luther King Jr Hwy Lanham, Jijini Maryland likiwa ni tukio maalum na la kipekee kwa wanachama wa CCM chini ya kauli mbiu ya CHANA GWANDA NA GAMBA, VAA UZALENDO

No comments: