Monday, December 31, 2012

2012...SHUKRANI. 2013, SHUKRANI ZAIDI

Hivi majuzi niliandika kwenye ukurasa wangu wa Facebook kuwa...
"Kama SABABU PEKEE ya wewe kutomshukuru Mungu ni kwa kuwa huna "la maana" uliloepuka mwaka huu, basi ujue kuwa UNATAKIWA KUMSHUKURU KWA KUKUEPUSHA NA HAYO AMBAYO WENZAKO "WANAMSHUKURIA" Yaaniiii.... UNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU MUNGU. Iwe kwa lile alilokuepusha, ama kukuepusha na lile waliloepuka wenzako."
Ndio...... MWAKA 2012 unakamilika.
Ni mwaka ambao ulijaa BARAKA kwangu. Hii haimaanishi kuwa haukuambatana na CHANGAMOTO.
Lakini ni katika changamoto hizo, nimeweza kukutana na UPENDO NA BARAKA ZA KWELI MAISHANI. Kukutana na WANIPENDAO na kusimama nami kwa dhati katika harakati zangu za maisha
Pengine, mwaka 2012 unaweza kuwa "mwaka mmoja wenye mkusanyiko wa mengi mema" kwangu kuliko mwaka wowote wa karibuni.
Na namshukuru Mungu kwa hilo.
Kwanza, NAMSHUKURU MUNGU kwa UHAI alionijaalia. Hili ni kuu zaidi kwani ni kwa uhai huu ndio nitaweza kueleza yote niliyopata mwaka huu.
Namshukuru kwa FAMILIA yangu ambayo amenijaalia.
Ile iliyo Tanzania na hii ya hapa. Kwa familia niliyokulia na hata aliyokulia anayenikuzia "baraka" zetu za sasa.
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata muda na Mama mzazi,
........ ambaye amekuwa nasi katika harakati za "mapokezi" ya binti yetu ambaye naye amewasilia 2012
Ongezeko jipya katika familia 2012. Asante Mungu kwalo
Lakini pia NAMSHUKURU MUNGU KWA CHANGAMOTO (wengine huita matatizo) ambazo kwa hakika ZIMENIFANYA NIWATAMBUE WAPENDWA WANGU WA DHATI.
Huu ni mwaka ambao NIMELIONA PENZI KULIKO MWAKA MWINGINE WOWOTE.
Na najivunia na kumshukuru Mungu kwa hilo.
Lakini pia, mwaka huu umekuwa na mafanikio ya "kikazi" ambapo, kwa ushirikiano na Kaka Mkubwa Abou, na uwezeshwaji wa VIZION ONE, tumeweza kujipatia vifaa vya kisasa vya kazi na sasa mipango ni kuuanza mwaka kwa harakati kabambe za kuiELIMISHA, BURUDISHA NA KUIKOMBOA JAMII yetu kupitia uwezeshwaji huu chini ya JAMII PRODUCTION
Abou Shatry na "silaha" kuu ya Jamii Production
Nashukuru Mungu kwa MARAFIKI WENGI niliowapata.
Si wengi kwa idadi tu, bali kwa UBORA.
Nimetambuana na wengi na hasa kupitia KAZI nifanyazo, na nashukuru Mungu kwa kila mmoja.
Nimalizie kwa kusema NAMSHUKURU MUNGU KWA NAMNA AMBAVYO MWAKA 2012 UMEKUWA na pia namshukuru kwa KILA CHANGAMOTO ALILONILETEA kwani kwalo nimedhihirika kwa wengi.
Namshukuru kwa WASOMAJI WANGU WOTE (ambao kwa namna moja ama nyingine nimewaweka kando kusaka maisha zaidi) ambao pia nawaahidi kurejea punde kuendeleza MIJADALA kila uchao.
Kwa mwaka huu 2012 unaoisha, NAMSHUKURU MUNGU KWAWO. Na kwa 2013, NAMSHUKURU ZAIDI KWA NAMNA NITAKAVYOUKABILI.

HAPPY NEW YEAR 2013

1 comment:

Mija Shija Sayi said...

Mungu ni mwema sana kaka Mubelwa..

Mimi ninawatakieni kila la heri katika kila jema mtakalolifanya au hata kuliwaza...

Mwaka 2013 ukawe ni mwaka wa mafanikio sana kwenu na wote watakaopitia blogu hii..

Salamu zangu kwa wote, Bibi Pau, Mama Pau, mdogo wake Pau, na Jamii production yote..

Jamii Production is doing an amaizing job...

Happy new year to you all...