Sunday, March 3, 2013

Kenya...MTACHAGUA VIONGOZI WENU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

Leo (March 4, 2013) wananchi wa Kenya wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya KATIBA MPYA.
WaKenya wamesikiliza kampeni za muda mrefu toka kwa wagombea wajazao nafasi mbalimbali.
Swali kwa ndugu zangu waKenya ni kuwa, mmeshajiuliza mtamchagua nani kuwa rais katika uchaguzi ujao?
Hapa sisemi kuchagua kwa jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Na je! Ndugu zangu wa Kenya mmeshajiuliza kuwa mnataka kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi?
Ama mliwasubiri waje na UONGO WAO ndio muanze kujipanga jinsi ya kukubaliana na uongo wao?
Ama mpaka waje na pesa ndio muangalie namna zinavyoweza kuwafaa?
Natumai hamkusubiri waje kuwaambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwenu.
Ama hamkusubiri waje na takwimu njema zisizoeleza mlivyo na kisha kuwaaminisha kuwa mnawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yenu.
Je!! Umeshawasiliana ama kujadiliana na yeyote masuala haya?
Nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
MTACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

1 comment:

emuthree said...

Twawatakia kila laheri, na sisi tukilijua hilo kuwa mwenzako akinyolewa na weye tia maji kichwa chako, kwani zamu yako inakuja.