Sunday, June 16, 2013

HAPPY FATHER'S DAY.....GOOD PAPA(s)


image from Stitches, Scraps and Sparkles in the Sun
"Role modeling is the most basic responsibility of parents. Parents are handing life's scripts to their children, scripts that in all likelihood will be acted out for the rest of the childrens' lives."--
Stephen R. Covey. Siku kama ya leo kila mwaka huadhimishwa kuwakumbuka, kuwashukuru, kuwaheshimu na kuthamini mchango wao katika maisha ya wengi.
Nami nachukua nafasi hii kumshukuru na kumuombea Baba yangu mpendwa ambaye amekuwa na bado ni ROLE MODEL wangu maishani.
Wanasema mtoto kwa Baba hakui. tangu nabebeka kwa mkono mmoja mpaka sasa, AKINGALI BABA KWANGU
Lakini pia najua kuwa Babangu amekuwa alivyo na amenilea kwa misingi myema kwa kuwa alilelewa vema na Babake. Wako wengi ambao wana wazazi japo wazazi hao hawaonekani kuwa na msaada kwa maisha yao, lakini wapo wazazi ambao walitumia muda wao mwingi "kuwekeza" katika maisha ya watoto wao na sasa wametangulia mbele ya haki lakini wametuachia HAZINA kubwa ya busara na maisha mema.
Nami leo napenda kuungana na ndugu wote ambao walipata malezi bora na mema toka kwa Baba zao lakini kwa mapenzi ya Mungu wametangulia mbele za haki. Hawa wana kila sababu ya kukumbukwa na kuenziwa na leo napenda kuungana na Luciano katika kuwakumbuka, kuwaombea na kuahidi kuendeleza mema yote waliyotufunza kupitia wengine.
Msikilize aliloambiwa Luciano asemapo "what you make out of life, he said, depends on what you put-in, my child".
Ndio usia alioupata toka kwa Babake na naamini wengi wameambiwa haya.
Kwa wenzangu ambao ni ma-BABA na bado wana BABA ZAO, basi ni mchanganyiko wa MSAADA NA DENI kwa kuwa kwa kutokukua mbele ya Babako, ukingali mwana, na kwa kuwa Baba, una deni la kuonyesha yale mema uliyotendewa na sasa unastahili kuyatenda kwa wanao.
Nami nikabarikiwa na wangu wa kwanza Paulina  '09
Kisha jukumu la pili Annalisa '12
 Na tuwakumbuke na kuwaenzi kinababa ambao wanatupenda na kuwekeza kwetu.
Tuwakumbuke na kuwaenzi wale waliotufanya tuwe tulivyo.
Tuwakumbuke waBABA wote ambao si waBABA kwetu kwa kuwa wametuzaa, bali kwa kuonyesha njia katika maisha yetu.
Wapo wengi ambao kwa mipango yao ama ya Mungu hawana watoto wao, lakini maisha yao yamekuwa MWONGOZO kwa watoto wengi.
Na hawa...NI WAZAZI (kutokana na ulezi wao)
Kama nilivyoandika  kwenye ukurasa wangu wa FACEBOOK.....
"Huwi BABA kwa "kuzalisha" bila kulea.
Na....
Waweza kuwa BABA kwa KULEA hata asiye UZAO WAKO
Kwa hiyo..
UNALEA kwa kuongoza, kuelekeza, kukanya na ZAIDI KWA KUWA MFANO KUPITIA MAISHA UISHIYO.
Kwa mantiki hiyo...
Kila anayeishi ni MLEZI kwa mfumo wake wa maisha.
Na si tumesema...
Kuwa kwa kulea unakuwa BABA?
Basi...
HAPPY FATHERS 'DAY KWA WABABA WOTE WEMA.
Waliopata hadhi hiyo kwa HIARI ama LAZIMA.
Waliopata hadhi hiyo kwa KUDHAMIRIA ama "BAHATI MBAYA"
Waliopata hadhi hiyo kwa MALEZI WATOAYO ama WAFUATILIWAVYWO NA WATOTO WA WENZAO.
Kumbuka....
Kila utendalo maishani ni FUNZO.
UZURI ama UBAYA wa funzo lako litatokana na utendalo.

Happy Fathers' day
"

Na wimbo huu ujao ni wazazi ambao walitupenda saaana, wakawekeza saaana na kisha wakamaliza kazi na kutangulia mbele ya haki. Nao leo hii NAWAKUMBUKA NA KUWATHAMINISHA
 Ni GOOD PAPA toka kwake LUCIANO.
NB: Ninalojifunza toka kwa Luciano ni kuwa haijalishi BABA alikuwa na maisha ya kiwango gani, bali amefanya nini maishani. Changamoto yetu hapa ni kujiuliza kuwa tunawaenzi vipi kinaBaba zetu na kwa sisi Baba watarajiwa tunajiandaa vipi kuwalea wanetu?
JUMAPILI NJEMA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA !!

emuthree said...
This comment has been removed by the author.
emuthree said...

HONGERA MKUU KWA KUWA BABA MWEMA