Sunday, October 20, 2013

TAHADHARI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI

Sasa wanatumia mitandao ya Internet ya Kuomba ajira
Kwa hisani ya mdau Henry Kapinga

Kuna UTAPELI mpya umeingia nchini Tanzania.
Watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo hutangazwa kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa.

Matukio yenyewe yanakuwaje?
Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai  wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho.

Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.

Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli.

KUWA MAKINI EWE MTANZANIA

No comments: