Monday, February 17, 2014

Mabinti wa kiTanzania hapa DMV watembelea studio za Jamii Production

Mmoja wa watayarishaji na watangazaji wa Jamii Production Mubelwa Bandio akitoa maelezo ya namna vipindi vinavyorekodiwa na / ama kurushwa moja kwa moja toka studio za Jamii Production
Jumamosi ya Feb 17, 2014, mabinti wa kiTanzania waishio hapa DMV Belina Mushala, Olivia Mutalemwa na Angelina Mushala walitembelea studio ya Jamii Production kujifunza namna tunavyofanya kazi.
Baada ya kumaliza ziara hiyo, waliketi chini KWA MAZUNGUMZO na Harriet "Titty" Shangirai kujadili masuala mbalimbali kuhusu elimu ya Tanzania na Marekani ambako kote wameishi. Kuna mengi mema ya kujifunza kutoka kwao
Karibu uungane nasi
Wazazi wa mmoja wa binti hao, Bwn na Bibi Pius Mutalemwa wakifuatilia jambo pamoja na Harriet Shangirai (kulia)

Mazungumzo
Jamii Production inawashukuru mabinti hawa na wazazi wao, na pia itaendelea kuwa wazi kwa wale wote wenye lengo la kutaka kujifunza kitu kutoka kwetu.

No comments: