Sunday, March 16, 2014

Father Evod Shao azungumzia mwaka mmoja wa Papa Francis katika kipindi cha NJE-NDANI

Wiki hii, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, alitimiza mwaka mmoja tangu achaguliwe kutwaa nafasi hiyo.
Na kwa miezi yote 12 iliyopita, Papa Francis amekuwa mmoja wa watu waliofuatiliwa zaidi duniani na kuaminika kuwa mmoja wa watu waliokuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka wa 2013.
Papa alitawala habari kwa kuonyesha nia ya kulifanya kanisa kuondokana na dhana ya utajiri na hata kushirikisha wale ambao kwa mtazamo wa wengi walionekana kutengwa na kanisa.
Kuweza kujua kuhusu mwaka wa kwanza wa Papa, nimezungumza na Padri Evod Shao wa Kanisa katoliki anayehudumu hapa Washington DC na kwanza nikamuomba aeleze anavyouchukulia mwaka wa kwanza wa Papa Francis

No comments: