Wednesday, June 11, 2014

Usikose kusikiliza kipindi cha NJE-NDANI wiki hii


Mubelwa Bandio akimhoji Fabian Lwamba wa KRYSTAAL
Katika NJE-NDANI wiki hii kati ya utakayosikia mahojiano na Fabian Lwamba
Mmoja wa ndugu watatu wanaounda kundi la KRYSTAAL ambao walizaliwa kwenye familia iliyojiweza, lakini mgogoro wa kisiasa ukawafanya waikimbie Zaire na kutengana.
Michael, Fabian na Alistone Lwamba wanaounda kundi la KRYSTAAL
Walikuja kuungana Canada ambako kwa miaka 16 wamekuwa pamoja kama kundi la muziki wa injili
Wametoa albamu 6 na kupata tuzo 26
Pia utamsikia ripota wetu Sebastian Atilio ambaye amerejea kutoka safari ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Sebastian Atilio na wenzake wakiwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro
Aliona nini huko? Alijifunza nini? Ni kipi alichogundua kama udhaifu mkubwa kwenye rasilimali zetu huko?
Yote haya na mengine mengi ni kwenye NJE-NDANI na Mubelwa Bandio, Jumamosi kuanzia saa 6 kamili kwa saa za Marekani mashariki (NOON EST) kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com

No comments: