Thursday, January 1, 2015

Funga mwaka ya Jumuiya DMV yafana

 Aliyekuwa mwakilishi wa Diaspora bunge la katiba Mhe. Kadari Singo akielezea shughuli za bunge hilo na jinsi gani alivyopigana kutetea swala la uraia pacha huku akiwasihi wanaDiaspora kubadili mtizamo wao kwa nchi yao.
Mwakilishi wa maswala ya uhamiaji Bi. Fatmata Barrier akifafanua sera ya uhamiaji ya Obama kuhusiana na kutoa vibali vya kazi kwa wasiokua na makaratasi kwenye sherehe ya mkesha ya Jumuiya ya Watanzania DMV iliyofanyika Lanham, Maryland Jumamosi Desemba 31, 2014.
Mgeni Rasmi Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali (wapili kushoto) akiwa pamoja na Balozi Mstaafu Mhe. Mustafa Nyang;anyi, Rais wa Jumuiya ya Wanzania DMV bwn. Iddi Sandaly na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka.
 Watanzania wakifuatialia wasemaji wa maswala mbalimbali yakiwemo maswala ya bunge la katiba na maswla ua uhamijai kwenye sherehe ya kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Oxford Center uliopo Lanham, Maryland.
Mwenyekiti wa CCM tawi la DMV bwn. George Sebo akiwa na mkewe Aunty Grace(kulia) wakiwa na wageni wao kwenye sherehe ya Jumuiya ya Watanzania DMV ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyia Lnham Maryland nchini Marekani.

Bwn. Jacob Kinyemi na mama mwenye nyumba wake na wakijumuika na wanajumuia wengine katika kusherehekea kuukaribisha mwaka 2015.
kwa picha zaidi bofya soma zaidiNo comments: