Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC na vitongoji vyake umeanza Jumamosi ya Januari 24, 2015.
Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza nasi kwa ufupi kuhusu darasa hilo.
Karibu umsikilize
|
Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang'anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania hapa DMV Said Mwamende |
|
Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo |
|
Baadhi ya wazazi waliokuwa ndani ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo |
2 comments:
Nimevutiwa sana na taarifa hii. Mnachofanya wenzetu huko DMV katika suala hili la kufundisha ki-Swahili ni mfano uliotukuka, mfano wa kuigwa. Hongera zenu, na nawatakia mafanikio bila kikomo.
Post a Comment