Dar es Salaam, Tanzania , August
11, 2015 :
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited leo imemtangaza Mkurugenzi wake mpya Bw. Ian Ferrao anayechukua nafasi ya Mkurugenzi anayeondoka Rene Meza ambaye hivi karibinu aliteuliwa kuwa Aisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ooredoo Myanmar kuanzia mapema mwezi ujao.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited leo imemtangaza Mkurugenzi wake mpya Bw. Ian Ferrao anayechukua nafasi ya Mkurugenzi anayeondoka Rene Meza ambaye hivi karibinu aliteuliwa kuwa Aisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ooredoo Myanmar kuanzia mapema mwezi ujao.
Ferrao kwa sasa hivi ni Mkurugenzi Mtendai wa
Vodacom Lesotho.Ana uzoefu mkubwa wa uongozi katika sekta ya mawasiliano katika
nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika.Kabla ya kjiunga na Vodacom Lesotho alikuwa
Afisa Mtendaji Mkuu anayesimamia biashara za kampuni ya Vodacom barani Afrika na alikuwa na hisa
katika kampuni ya Africonnect ya nchini Zambia.Ujio wake kuongoza Vodacom
Tanzania ni kama vile amerejea nyumbani kwa kuwa wazazi wake waliwahi kuishi
nchini tangu mwaka 1952 kabla ya kuhamia nchini Uingereza mwaka 1970.
Akiongelea
uteuzi wake alisema “mimi ni mzoefu na nina ujuzi wa kuongoza sekta ya
mawasiliano na nina imani sekta hii ni zaidi ya mwasiliano bali imeonyesha
mabadiliko makubwa katika kuchangia kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa
kuboresha maisha ya watu na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi.Nina
imano Vodacom ina uwezo wa kuendelea kuboresha mawasiliano nchini
na kuzidi kufanya maisha ya watanzania kuwa murua”
Naye Rene Meza Mkurugenzi aliyeiongoza Vodacom
Kuanzia mwaka 2011 alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake Vodacom
Imefanya mabo mengi katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini ikiwemo kukua
kwa mtandao huo na kuwa na wateja zaidi ya milioni 12 na kuanzishwa kwa huduma
ya M-PESA ambayo inatumiwa na wananchi wengi Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi
zenye watumiaji wengi kwenye huduma hii kwenye makampuni ya Vodacom Group.
No comments:
Post a Comment