Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu katika viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.[/caption] MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema awamu ya Serikali ya Tano itakayoundwa na CCM itakuwa maalum kwa ajili ya ujenzi na ufufuaji wa viwanda nchini ili kuongeza nafasi ya ajira kwa vijana na kuinua kwa kasi uchumi wa nchi. Bi. Suluhu ameyasema hayo alipokuwa akiinadi ilani mpya ya Chama Cha Mapinduzi katika ziara ya kampeni ya jijini Dar es Salaam ya kuinadi ilani hiyo kwa wananchi juu ya nini Serikali ya CCM itafanya endapo itapewa ridhaa tena na wananchi kuunda Serikali na kuongoza nchi baada ya uchaguzi. Alisema watahakikisha wanajenga viwanda na kuvifufua vile vilivyokufa ikiwa na lengo la kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na hapo hapo kuwatambua wafanyabiashara ndogondogo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo katika biashara zao. "...Tunataka awamu ya Serikali ya Tano iwe awamu ya viwanda...tunataka asilimia 40 ya ajira ipatikane kwenye sekta ya viwanda...," alisema mgombea mwenza.
Bi. Anna Abdallah akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Samuel Sitta akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Burudani yake Isha Mashauri mara baada ya kusikiliza ilani ya CCM kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji akichukua taswira ya mkutano huo kwa simu yake kwa ajili ya kumbukumbu.
Alisema pamoja na hayo Serikali itakayoundwa na CCM itaanzisha dawati maalumu la bodaboda na bajaji na kukamilisha usajili wa vikundi vyao ili kuangalia namna ambayo kundi hili la vijana linaweza kufanya shughuli zao bila kubughuziwa.
Alisema uimarishaji huo wa madawati ya bodaboda na bajaji utaenda sambamba na kuongeza mipaka ya kufanyia kazi, kutambua bodaboda na bajaji kwa rangi kulingana na maeneo zinapofanyia kazi ili zitambulike kwa uraisi.
Alisema ili kumaliza kero ya foleni na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya kisasa pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la Kibaha ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es Salaam kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa barabara ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni katika barabara kubwa.
Aidha Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili kupunguza msongamano katika barabara kubwa.
Alisema ili kuboresha huduma za afya jijini Dar es Salaam, Serikali ya CCM kupitia ilani yake itaiongezea hadhi na kutoa upendeleo kwa Hospitali ya Mwananyamala ikiwa ni pamoja na kuiongezea watumishi wa kada zote pamoja na mgao wa dawa kulingana na mahitaji yake.
Alisema mbali na hapo ilani inaeleza watahakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na kuhimiza kuwakatia bima wananchi ili waweze kupata huduma hiyo muda wote bila kujali uwezo wa vipato vyao.
Aliongeza wafanyabiashara nao hawajasahaulika kwani imetenga maeneo sehemu mbalimbali ya ujenzi wa masoko kwa wafanyabiashara ndogondogo, ambapo nafasi takribani 3263 kwa eneo moja zitapatikana na kupewa wafanyabiashara ndogondogo huku jitihada kama hizo zikiendelea maeneo mengine.
Kwa upande wa huduma za upatikanaji maji safi na salama zimepewa kipaumbele pia ambapo mradi mkubwa wa kutoa maji Ruvu Juu na Ruvu Chini pamoja na ule wa Mto Ng'ombe utamaliza kabisa kero ya maji kwa jiji la Dar es Salaam baada ya mwaka mmoja ujao. Mgombea huyo wa urais anaendelea na ziara yake mkoa wa Dar es Salaam kunadi ilani ya CCM.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment