Wednesday, September 2, 2015

ZANZIBAR STARS YAINGIA MASHINDANO YA KOMBE LA EAST AFRIKA DIASPORA DMV

Kwa mara nyengine tena timu ya Zanzibar Stars Diaspora Nchini Marekani, imejianda rasmi katika mashindano ya Mpira wa Miguu Diaspora Afrika Mashariki DMV, itakayofanyika mwishoni mwa juma hii Jumapili Sept 6, ambayo ni sikukuu ya wafanya kazi ijulikanayo kama (Labor day). 
Kikosi cha timu ya  Zanzibar Star Diaspora Nchini Marekani 
Burudani ya michuana hiyo imeandaliwa rasmi, (Kaka DC & DMV  East  Africa Diaspora Community Features) na katika michuano hiyo time (4)  zilizowakilishwa  Kenya,  Tanzania Stars, Zanzibar Stars na Rwanda.
Tukumbuke burudani ni ya siku moja, na Mechi ya kwanza itaaza rasmi, Majira ya Asubuhi  Saa (10:00am hadi 11:30am), ambapo
Group A: - Tanzania Stars itachuana vikali na timu ya Rwanda
Na kuazia Asubuhi ya Saa 11:30am hadi Mchana1:00pm ni
GROUP B: - KENYA vs ZANZIBAR
Katika Mshindi atakaepatikana hapo yaani FINALS itachezwa Mchana wa saa 2:00pm hadi 5:00pm. Michuano hii inafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho siku ya Wafanyakazi nchini Marekani.
Nyote mnakaribishwa kuangali burudani ya aina yake kwa wale wapenzi wa mchezo wa Soka.
ANUANI: FAIRLAND RECREATIONAL PARK
3928 GREENCASTLE RD. BURTONSVILLE, MD. 20866.

No comments: