Jumamosi Jan 14, kiongozi wa kampeni ya kuinua maadili kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge akishirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington alizindua kampeni hiyo yenye lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa.
Kampeni hiyo imeanza rasmi na itaendelea hadi mwezi Desemba mwaka huu ikijikita zaidi katika kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.
No comments:
Post a Comment