Darasa linakukumbusha kuwa...…
Watu watatu ni mimi na wewe.
Watu kumi ni mimi na wewekwa sababu kuna watu tumesimama nyuma yao. Lakini pia, ni watu wetu wa karibu wanaosimama nyuma yetu.
Mtu wa kwanza ni yule ambaye anapokuwa na kitu cha kutimiza hasubiri watu wakimbie pamoja naye. Huchakarika kadiri ya uwezo wake bila kulalamika wala kuvunjika moyo kwa kuwa hana msaada.
Mtu wa pili ni yule ambaye anapokuwa na jambo lake ni lazima apate msaada ndiyo alifanye kwa kasi. Mtu wa hivi bila kusukumwa haendi wala hawajibiki ipasavyo. Ni ngumu kutimiza mambo yake ipasavyo bila kuegemea wengine.
Mtu wa mwisho ni yule ambaye ni mlalamishi. Hutaka jambo lake watu wote waache shughuli zao kwa ajili yake. Hata kwenye ambayo ni wajibu wake kwanza, hulazimisha wengine kuwajibika kwa ajili yake, ama sivyo hununa au huzira na hata kuvunja ukairbu na mtu kwa sababu tu hakusaidiwa jambo ambalo ni wajibu wake.
Wale watu 10 nyuma ya watu. kila mmoja ajitafakari anavyowatendea watu wake wa karibu pale wanapotegemea sapoti yake.
Tujiulizetunaangukia kwenye kundi gani?
Darasa linakutakia tafakuri njema.
Thursday, September 7, 2023
Friday, August 11, 2023
Darasa 38: Hakuna asiye na cha kutoa na hakuna asiyehitaji
Darasa linakukumbusha kuwa.......…
Usiache kuwa jambo zuri kwa watu wengine hata wakati ule unapopitia magumu yako. Kuna watu wanaishi maisha ya kulalamika kila siku. Wao hivi wao vile. Kuna watu ni wenye kujiona wanastahili kupokea tu na si kutoa kwa sababu hawana pesa, au hawana hiki au kile. Kuna watu wamejipa hatimiliki ya kutendewa mema na si kutenda.
Rafiki, hata katikati ya magumu yako nenda ukawe jambo zuri kwa mtu. kuna namna nafsi yako itainuka. Kuna baraka utaichota. Nenda kawe jambo zuri kwa mtu. Kwa maneno au vitendo; kwa maneno na vitendo. Kaweke tabasamu usoni pa mtu.
Darasa linakutakia tafakuri njema.
DARASA la Laura Pettie ni makala zinazokujia kila Jumanne na Alhamis kupitia akaunti yetu ya YouTube. Unaweza kusikiliza makala zote kwa leo kubofya PLAYLIST HII au tembelea akaunti yetu hii ya YouTube
Mawaidha ya ijumaa 11.8.2023 "Mazuri tunayo yakosa kwa kuchelewa kuswali jamaa"
Leo kwenye mawaidha ya ijumaa 11.8.2023 unatazama hotuba kutoka kwa Sheikh Salim Mubaraka Sazi wa masjid Abuu-bakari uliopo Mlandege Manispaa ya Iringa, akitukumbusha kuhusu "mazuri tunayoyakosa kwa kuchelewa kuswali jamaa".
Monday, April 19, 2021
255 Info Package ya Kwanza Radio EP06 Aprili 19, 2021
Karibu kwenye show kabambe yenye muziki na habari mbalimbali za muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Mr Presenter anakupitisha kwenye taarifa mbalimbali za kimuziki ikiwemo mgodi wenye habari mbalimbali za muziki na wanamuziki wa Bongo Flava.
Leo atasikika mkongwe Adili Chapakazi, wasanii G-Nako, Hamadai, Iddo the Gold na Moni Centrozone
Ni kila Jumatatu saa kumi kamili kwa saa za Afrika Mashariki, na marudio ni saa kumi kamili kwa saa za Marekani ya Mashariki.
Kwanza Radio itapatikana punde online saa 24 kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com
Kwa sasa tusikilize kupitia
Radio Garden
radio.garden/listen/kwanza-radio/ZUtbxgBv
OnlineRadio Box
onlineradiobox.com/us/kwanza/?cs=us.kwanza
TuneIn
tunein.com/radio/Kwanza-Radio-s290047/
Sunday, April 18, 2021
AFRO KWANZA ya Kwanza Radio EP06 Aprili 17, 2021
Karibu kwenye show ya muziki wa kiAfrika ikiandaliwa na Mussa Yusuph.Leo utapata habari zaidi juu ya wasanii Oliver Ngoma, Tshala Mauna na Awilo Longomba.
Kipindi hiki hukujia kila Jumamosi kuanzia saa kumi kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na marudio ni saa kumi jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki.
Tutakujia punde kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com
Kwa sasa unaweza kusikiliza radio kupitia
Radio Garden
http://radio.garden/listen/kwanza-radio/ZUtbxgBv
OnlineRadio Box
https://onlineradiobox.com/us/kwanza/?cs=us.kwanza
TuneIn
https://tunein.com/radio/Kwanza-Radio-s290047/
Kama umekikosa, basi punde baada ya kupindi, bofya https://soundcloud.com/kwanzaproduction/afro-kwanza-ya-kwanza-radio-ep06-aprili-17-2021 https://soundcloud.com/kwanzaproduction/afrokwanza-ep05
Saturday, April 17, 2021
DONDOO NA REGGAE ya Kwanza Radio. Kazi za Lucky Dube
Jambo ambalo bado nawaza kuhusu Lucky Dube ni uwezo wake wa kuwaza kitu ambacho kipo, na ambacho kingeweza kutendeka kwa namna fulani lakini hakikutendeka hivyo japo kinaleta maana halisi ya fikra ya kutendeka kwake.
Yaani alikuwa na uwezo mkubwa saana wa KUSADIKI habari ama tukio ama maisha halisi kwa namna ambavyo yanaweza KUSADIKIKA.
Alieleza, kuuliza ama kufafanua utata ama fumbo ama mwenendo fulani wa maisha kwa namna ya kipekee.
Tunaweza kuangalia baadhi ya nyimbo kuwaza kwa pamoja kuwa ALIWAZA NINI??
Tutakujia punde kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com
Kwa sasa unaweza kusikiliza radio kupitia
Radio Garden
OnlineRadio Box
255 Info Package ya Kwanza Radio EP05 Aprili 12, 2021
Mr Presenter anakupitisha kwenye taarifa mbalimbali za kimuziki ikiwemo mgodi wenye habari mbalimbali za muziki na wanamuziki wa Bongo Flava.
Leo atasikika mkongwe Adili Chapakazi, wasanii G-Nako, Hamadai, Iddo the Gold na Moni Centrozone
Ni kila Jumatatu saa kumi kamili kwa saa za Afrika Mashariki, na marudio ni saa kumi kamili kwa saa za Marekani ya Mashariki.
Kwanza Radio itapatikana punde online saa 24 kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com
Kwa sasa tusikilize kupitia
Radio Garden
OnlineRadio Box
TuneIn
Reggae Time ya Kwanza Radio.. Rastafarianism
Amani, Upendo na Heshima kwako msikilizaji wa Kwanza Radio. Karibu katika kipindi hiki cha Reggae Time, kinachokujia kutoka hapa Kilimanjaro Studios. Na leo, tunagusia mambo kadhaa ambayo ni vema kuyajua kuhusu maRasta.
Watu wengi wanaposikia neno RASTAFARI, wanaelekeza fikra zao kwa watu wenye rasta ama dreadlocks, kwa uvutaji wa bangi, kwenye muziki wa Reggae na kadhalika.
Lakini, kwa hakika uRasta ni falsafa makini ambayo huchukua mwelekeo mkubwa wa kiImani.
Japokuwa wapo wengi ambao hufuata ama kujiita maRasta ili kupata mwanya wa kufanya baadhi ya mambo maovu, ukweli unabaki palepale kuwa wapo wafuasi wazuri wa imani ya uRasta, ambao jamii isiyowajua vema, inawachukulia visivyo.
Mubelwa Bandio anakusihi uwe naye pamoja mpaka mwisho.
Wewe msikilizaji unaweza kushiriki kwa kutuma ujumbe ama maoni yako kwenye mitandao yetu ya kijamii. Tufuatilie kwenye Facebook, Instagram, Twitter na Soundcloud. Tafuta Kwanza Production.
255 Info Package ya Kwanza Radio EP04 Aprili 4, 2021
Karibu kwenye show kabambe yenye muziki na habari mbalimbali za muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Mr Presenter anakupitisha kwenye taarifa mbalimbali za kimuziki ikiwemo mgodi wenye habari mbalimbali za muziki na wanamuziki wa Bongo Flava.
Leo atasikika mkongwe Adili Chapakazi, wasanii G-Nako, Hamadai, Iddo the Gold na Moni Centrozone
Ni kila Jumatatu saa kumi kamili kwa saa za Afrika Mashariki, na marudio ni saa kumi kamili kwa saa za Marekani ya Mashariki.
Kwanza Radio inapatikana online saa 24. Tusikilize kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com
Pia unaweza kusikiliza radio kupitia
Radio Garden
http://radio.garden/listen/kwanza-radio/ZUtbxgBv
OnlineRadio Box
https://onlineradiobox.com/us/kwanza/?cs=us.kwanza
TuneIn
https://tunein.com/radio/Kwanza-Radio-s290047/
Subscribe to:
Posts (Atom)